Ujenzi wa Maktaba kwenye shule ya Sekondari Nguva ulianza tarehe 27/03/2019 kwa fedha kutoka serikali kuu za malipo kulingana na matokeo( PAY FOR RESULT) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Hadi sasa ujenzi umekamilika ambapo fedha kiasi cha milioni 50 zimetumika na jengo linasubiri samani kwaajili ya matumizi. Aidha kukamilika kwa jengo hili la Maktaba kutawawezesha wanafunzi wa Shule ya Nguva ambayo ndiyo pekee yenye kidato cha tano na sita kupata mazingira mazuri ya kujisomea na kujifunza kutoka kwenye vitabu mbalimbali vya kitaaluma vitakavyokuwa vinapatikana kwenye Maktaba hiyo. Hali hii itawawezesha wananfunzi kukua kitaaluma na kuwapa morali ya kujisomea vitabu.
![]() |
![]() |
Muonekano wa Maktaba kwa nje
|
|
![]() |
![]() |
Muonekano wa maktaba kwa ndani
|
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa