UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII NA VIJANA KUPITIA SEHEMU AU “SECTIONS” ZAKE KATIKA IDARA
I. UKIMWI
Sehemu ya ukimwi inajishughulisha, kuratibu na kusimamia masuala ya ukimwi, katika suala hili idara inashirikiana na ASASI mbalimbali za nje na ndani ya nchi katika kupambana na maambukizi ya ukimwi mashirika hayo ni kama ifuatavyo: SAUTI, JHPIEGO, PSI, PASADA, TAYOA, UMATI, PATHFAINDER, PHARM ACCES ENGENDER,HEALTH, JSI, NA MDH. TEYODEN, MTANDAO WA ASASI MANISPAA YA KIGAMBONI, MTANDAO WA WALIOATHIRIKA NA VIRUSI VYA UKIMWI. Wadau hawa kwa pamoja na Manispaa wameweza kutoa elimu ya ukimwi, kipima mambukizi ya ukimwi, kutoa misaada ya vyakula kwa watu walioathirika na kutoa mafunzo kwa jamii kwa njia mbalimbali kama vijarida, sinema, mikutano, runinga na redio. Aidha, kuanzia mwaka 2017, Septemba hadi Februari, 2017. jumla ya watu 13443 walipimwa na kati ya hao 206 walikuwa na maabukizi ya virusi vya ukimwi sawa na asilimia 1.53. Aidha , Halmashauri kupitia bajeti yake ya mwaka 2017/2018 imetenga kiasi cha shilingi milioni 37.9 katika masuala yote yanayohusu ukimwi.
II. MIKOPO YA WANAWAKE NA VIJANA
Halmashauri ya Manispaa ya kigamboni inatoa mikopo ya wanawake na vijana kwa kupitia Benki ya DARES SALAAM COMMUNITY BANKI (DCB) ambapo kwa mwaka 2016/2017, Halmashauri ya Manispaa ya kigamboni imewekeza kiasi cha shilingi milioni 239 katika benki ya DCB. Aidha, katika mwaka wa 2017/2018 imetenga tena shilingi milioni 753 kwa ajili ya mikopo ya wanawake na vijana.
Idara ya maendeleo kupitia watumishi wake walio katika kila kata, huhamasisha wananchi kuunda vikundi vya watu watano watano walioafikana na kisha kuwasilisha Benki ya DCB, ambayo hutoa mafunzo ya uendeshaji wa biashara na taratibu za mikopo, vikundi vikikubaliana na masharti hupewa mikopo inayoanzia shilingi 250,000.00 hadi shilingi 350,000.00 kwa kila mwanakikundi. Hadi mwezi Februari, 2017 Halmashauri ya manispaa ya kigamboni imeweza kutoa mikopo kwenye vikundi 114 yenye thamani ya shilingi 161,500,000.00. na utoaji wa mikopo unaendelea.
III. VIJANA
Idara ya mendeleo ya jamii na vijana kupitia kitengo cha vijana na mtandao wa vijana KIYODEN (Kigamboni Youth development Network ). Mtanadao huu umeanzishwa ili kuleta umoja kwa vijana na kuanzisha vikundi mbalimbali vya kijamii na kiuchumi. Vijana, pia wanapatiwa mikopo kupitia Benki ya DCB, ikiwa ni nusu ya mkopo wote uliotengwa na manispaa. Aidha, hadi Februari, 2017 vikundi vya vijana 38 vimeweza kupatiwa mikopo kupitia DCB wenye thamani ya shilingi milioni 9.5. Idara imeweza kuhamasisha vijana ili waweze kuanzisha vikundi mbalimbali vya utamaduni, michezo ya kuigiza, uvuvi, kilimo na ufugaji wa samaki na vijana hivi sasa wameonyesha nia ya kuazisha vikundi hivyo, kupitia mtandao wa KIYODEN. Idara pamoja vijana imeanza kuandaa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2017/2018
IV. WANAWAKE NA WATOTO
Idara kupitia, dawati la jinsia na watoto imeunda mabaraza ya watoto mkatoka kata zote 9 ambao hukutana na kujadiliana matatizo wanayopata watoto katika sehemu mbalimbali kama mashuleni , majumbani n.k. Aidha, sehemu hii imeweza kishirikiana na sehemu ya mikopo katika kuhamasisha wanawake ili waweze kuunda vikundi na kujikwamua kiuchumu. Idara pia imeshirikiana na taasisi mbalimbali kama TBS katika kutoa mafunzo ya usindikaji vyakula.
V. TASAF (Tanzania Social Fund)
Halmashauri ya Manispaa hupata msaada wa ruzuku kwa familia duni kupitia mfuko wa TASAF wa kusaidia familia duni. Aidha, familia 1215 zinanufaika na msaada wa ruzuku hiyo, kupitia TASAF. Fedha hizi hupitia katika Halmashauri ya Temeke kwa sababu Halmashauri ya Manispaa ya kigamboni ni mpya na haina mkataba na TASAF.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa