Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila ametoa wito kwa Wakuu wa Wilaya za Kigamboni na Ubungo kutumia magari yanayotolewa na Serikali katika kuwahudumia Wananchi na kutatua kero mbalimbali katika maeneo yao.
RC Chalamila ametoa wito huo leo Septemba 22. 2025 katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kukabidhi magari mawili (2) aina ya Toyota Prado yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuwarahisishia wakuu wa Wilaya hizo kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
"Leo Wakuu wa Wilaya za Kigamboni na Ubungo mnakabidhiwa magari haya, naomba yakatumike kama chombo cha kuwahudumia wananchi." Alisema Mhe Albert Chalamila.
Aidha kwa upande mwingine amekabidhi gari aina ya Toyota crown kwa golikipa wa Timu ya Taifa la Tanzania (Taifa Stars) Ndugu. Yakoub Suleiman ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati robo fainali ya mashindano ya CHAN katika Mchezo kati ya Tanzania na Morocco ambapo licha ya kufungwa ameamua kukabidhi gari hilo ikiwa ni kutambua jitihada za golikipa huyo.
Kwa upande mwingine amewaagiza Maafisa Michezo wa Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam kuanzisha timu za mpira wa miguu za Wilaya ili kukuza vipaji na kutoa fursa za ajira kwa vijana katika Wilaya hizo.
Mpira wa miguu ni moja kati ya mchezo pendwa katika Taifa letu na umetoa fursa za ajira kwa vijana wengi wanaocheza ligi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa