WACHIMBAJI NA WASAFIRISHAJI WA MADINI YA UJENZI WATAKIWA KULIPA USHURU NA KODI ZA SERIKALI
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Ndugu, Erasto Kiwale amewataka wachimbaji na wasafirishaji wa madini ya ujenzi kuhakikisha wanafuata taratibu sheria na kanuni za ulipaji wa ushuru wa madini ili kuongeza mapato yatakayoiwezesha Manispaa kuboreshaji huduma za kijamii.
Ndugu, Kiwale ametoa wito huo leo Septemba 04. 2025 wakati akiongoza kikao cha Kamati ya mapato ambayo ilikutana viongozi wa wachimbaji na wasafirishaji wa madini ya ujenzi waliopo ndani ya Manispaa ya Kigamboni kwa lengo la kutoa uelewa juu ya utunzaji wa mazingira na ulipaji wa kodi za Serikali hususan ushuru wa madini.
Aidha amesema Manispaa haitamvumilia mtu yoyote atakaekwepa kulipa ushuru huku akiwataka viongozi hao kuwa mabalozi na kuhamashisha ulipaji wa shuru na kodi za Serikali kwa wachimbaji na wasafirishaji wanaowasimamia.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa