FURSA MBALI MBALI ZA UWEKEZAJI KWENYE ENEO LA KILIMO NA UMWAGILIAJI
Skimu ya Umwagiliaji Nyange ambayo inahitaji uwekezaji kwa kushirikiana wa wakulima waliopo eneo hili lenye ukubwa wa hektari 139.0 zinazofaa kwa kilimo .
Bustani iliyopo Gezaulole yenye ukubwa wa ekari ishirini na tano (25.0) ya kuzalisha miche na mazao ya aina mbalimbali
Uzalishaji wa mazao ya kilimo kwenye eneo la ukubwa wa hektari 21000 yanayotumiwa na wakulima na ziada kuuzwa kwenye masoko ya nje na ndani
MAZINGIRA YA HALI YA HEWA
Kwa ujumla hali ya hewa ni ya joto na hali ya unyevunyevu karibu kwa kipindi chote cha mwaka
Hali ya mvua
Kwa wastani mvua ni kati ya milimita 850 kwa mwaka. Mvua ni za misimu miwili ambapo mvua kubwa zimekuwa zikinyesha katikati ya mwezi Februari hadi Mei na mvua nyepesi hunyesha kati ya kipindi cha Oktoba hadi Januari. Kiwango cha mvua hizo ni 58.8% (508milimita) kwa miezi ya katikati ya Februari hadi Mei na kwa kiwango cha 41.2% (4725 milimita) kwa miezi ya Oktoba hadi Januari. Kipindi cha ukame ni miezi ya Juni hadi Septemba.
Hali ya joto
Kiwango cha chini cha joto ni 25oC, na kiwango cha juu ni 35oC na likizidi sana ufikia 38oC.
Hali ya unyevu (humidity)
Hali ya unyevunyevu huwa kati ya 38% hadi 93%
HALI YA KILIMO
Katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kilimo kinachofanyika ni ukulima wa aina mbili ambao ni kilimo cha pembezoni mwa mji (peri urban agriculture) na kilimo mjini (urban agriculture). Maeneo yanayolimwa ni yale ambayo yametengwa na wakulima kwa ajili ya kazi hii, pia katika sehemu ambazo hazijaendelezwa kwa kukodiwa na wakulima au kutumiwa na wanaozimiliki kufanya shughuli za kilimo. Hata hivyo, kadiri mji unavyokua wakulima wanalima kilimo mjini/maghorofani kwa kutumia vifaa mbalimbali ambavyo ni kama mifuko, ndoo, pia wana lima vijibustani vidogo pembezoni mwa makazi, kandokando ya barabara na sehemu zilizo wazi zinazosubiriwa kuendelezwa. Shughuli za kilimo zinachangia katika usalama wa chakula kwa kaya kwa kiwango cha asilimia 30%. Kaya zinazofanya shughuli za kilimo ni 3941 zenye wakulima 12120 na hektari zinazolimwa mazao mbalimbali zinakadiriwa kuwa ni 21000.
Kilimo cha mazao mbalimbali:
Mazao yanayolimwa kwa ajili ya chakula ni:
Muhogo, viazi vitamu, mpunga, mahindi, mboga mbalimbali zikiwa ni pamoja na mchicha, matembele, nyanya, mbaazi, mikunde, bamia, matango, nyanya chungu, kabeji mchina, bilinganya, pilipili hoho na kali na matunda mbalimbali yakiwa ni pamoja na embe,mapapai, matikiti maji, na mananasi.
Mazao yanayolimwa kwa ajili ya biashara ni:
Minazi, miembe, mikorosho, muhogo, viazi vitamu, mahindi, mpunga, mboga mbalimbali zikiwa ni pamoja na mchicha, matembele, nyanya, mbaazi, mikunde, bamia, matango, nyanya chungu, kabeji mchina, bilinganya, pilipili hoho, pilipili kali uyoga, na matunda ambayo ni michungwa, minanasi, mipapai, migomba, matikiti maji na mistafeli. Michikichi, maua, miti ya mapambo na vivuli, ukoka pia vinalimwa.
Eneo la kilimo:
Ukubwa wa maeneo yanayofaa kwa ajili ya kilimo cha mazao yaliyoainishwa ni kama ifuatavyo:
ZAO HEKTARI
1.Mpunga 3040.0
2.Muhogo 5120.0
3.Mahindi 500.0
4.Mboga 11,500.0
5.Minazi 360.0
6.Michikichi 480.0
JUMLA21000.0
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa