UTANGULIZI
Wilaya ya Kigamboni imeundwa kutokana na Wilaya mama ya Temeke na ni moja kati ya Wilaya 5 zinazounda Mkoa wa Dar es Salaam. Wilaya ya Kigamboni ilianzishwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 462 la mwaka 2015 kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi karibu zaidi.
ENEO LA WILAYA
Wilaya ya Kigamboni ina eneo la kilomita za mraba 577.9 sawa na hekta 57,786.8 na ukanda wa Pwani wenye urefu wa kilometa 65. Aidha Wilaya ya Kigamboni kwa upande wa mashariki inapakana na Bahari ya Hindi, kusini inapakana na Wilaya ya Mkuranga – Mkoa wa Pwani na upande wa kaskazini inapakana na Bahari ya Hindi na upande wa magharibi imepakana na Wilaya ya Temeke.
IDADI YA WATU
Kufuatia Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Wilaya ya Kigamboni ilikuwa na jumla ya watu 162,932 na kaya 40,133. Kati ya hao wanaume walikuwa 81,199 na wanawake walikuwa 81,733. Hadi kufikia Desemba mwaka 2019, Wilaya ya Kigamboni inakisiwa kuwa na wakazi wapatoa 238,591 kati yao wanawake ni 119,686 na wanaume ni 118,905 hii ni kutokana na ongezeko la asilimia 5.6 kwa mwaka.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa