Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mhe. @dalmiamikaya amewataka watendaji na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ndani ya Manispaa ya Kigamboni kuwashirikisha na kutoa elimu kwa wananchi juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao ili waweze kupata uelewa.
DC Mikaya ametoa agizo hilo leo, Agosti 8. 2025 wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miundombinu ya barabara katika Kata ya Mjimwema na Kibada aliyoifanya kwa lengo la kujionea hali ya utekelezaji wa miundombinu hiyo.
"Jukumu la viongozi wa Mitaa na Kata ni kutoa elimu na taarifa sahihi ili wananchi washiriki ipasavyo kwenye maendeleo ya Mitaa yao." Alisema DC Mikaya.
Aidha, ameiagiza Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) kutengeneza barabara za dharura zitakazowawezesha wananchi kupita wakati ujenzi na ukararabati unaendelea.
Pia ameiagiza wakala huo kuhakikisha wanawasimamia wakandarasi wote wanaojenga barabara ndani ya Wilaya ya Kigamboni na kuhakikisha wanakuwepo kwenye eneo la Mradi wakati wote ili kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu hiyo
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa