1.0 UTANGULIZI
Utoaji wa Elimu ya sekondari unazingatia vyema matakwa ya sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 2014 Tamko Na. 3:1:3 serikali itaweka utaratibu wa elimu msingi kuwa ya lazima kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne; na kutolewa kwa miaka kumi na umri wa kuanza darasa la kwanza kuwa kati ya miaka minne hadi sita kulingana na maendeleo na uwezo wa mtoto kumudu masomo katika ngazi husika na elimu hiyo itatolewa kwa umma bila ada kumwezesha mwanafunzi kupata ujuzi stahiki kulingana na mfumo wa Tuzo wa Taifa.
2.0 MAJUKUMU YA IDARA
i. kusimamia ufanyikaji wa mtihani ya utamilifuā na mitihani ya Taifa
ii. Kusimamia upatikanaji wa vifaa vya kufundishia nakujifunzia
iii. Kukusanya na kuhakiki takwimu za shule 20 za sekondari (TSS) 2016/2017
iv. Kusimamia upatikanaji wa miundombinu nasamani za shule za serikali. Kdhalika kukagua miundombinu, mazingira, hali ya samani na uendeshaji wa Taaluma katika shule za sekondari.
v. Kuandaa orodha na gharama za likizo ya malipo kwa watumishi wa idara ya sekondari
vi. Kuandaa mapendekezo ya walimu wa shule za serikali kupanda madaraja/vyeo kwa kila mwaka
vii. Kukusanya, kuhakiki na kuunganisha taarifa za MMES za kila robo ya mwaka kwa shule za sekondari za serikali na kuziwasilisha Mkoani na TAMISEMI
viii. Kuandaa na kuratibu wanafunzi wa shule za sekondari kushiriki mashindano ya michezo ya UMISETA ngazi ya shule hadi Taifa
ix. Kusimamia utekelezwaji wa Mitaala katika ngazi za shule
x. Kusimamia ujenzi ,ukarabati na upatikanaji wa miundombinu na samani za shule
xi. Kufanya makisio ya mahitaji ya walimu kimasomo
xii. Kusimamia na kufuatilia mapato na matumizi ya fedha katika shule
xiii. Kuwatambua wanafunzi wenye mahitaji maalum na kuwapa mahitaji husika
xiv. Kuwatambua wanafunzi wanaotoka mazingira magumuna na kuwapa msaada wa kielimu
Kufanya vikao na kuchukua hatua juu ya maauzi /makubaliano katika kuboresha Elimu ya sekondari.
3.0 HUDUMA ZINAZOTOLEWA
i. Kutoa miongozo na ushauri wa Elimu kwa wanafunzi na wazazi;
ii. Kusimamia na kupitisha uhamisho wa wanafunzi;
iii. Kutoa elimu kwa wanafunzi, wazazi na wananchi kwa ujumla juu ya umuhimu wa Elimu ya sekondari
4.0 ORODHA YA SHULE ZA SEKONDARI ZA SERIKALI ZILIZOPO KATIKA MANISPAA YA KIGAMBONI
KATA
|
JINA LA SHULE
|
---|---|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
5.0 MIRADI YA MAENDELEO MWAKA WA FEDHA 2023/2024
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa