Idaraya Mipango,TakwimunaUfuatiliaji inashughulikia upangaji na uratibu wa mipango ya maendeleo katika miaka husika, usimamiz ina ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ya Halmashauri, Tafiti na ukusanyaji wa Takwimu pamoja na kuratibu shughuli za Uwekezaji. Idara hii inaongozwa na Mchumi wa Manispaa na imegawanyika katika sehemu tano kamaifuatavyo:-
• Mipangona Sera
• Usimamizi na Ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo
• Uwekezaji
• Tafitina Takwimu.
Sehemu ya Mipango na Sera.
Majukumu ya sehemu hii ni kamaifuatavyo:-
• Kusimamia Uandaaji wa mpango wa utekelezaji waIlani ya uchaguzi kilamwaka.
• Kuratibu ufanisi wa mifuko ya Halmashauri: LGCDG, Mfuko wa Jimbo na fedha za mapato ya ndani.
• Uratibu na utayarishaji wa Mipango shirikishi katika Kata zote za Halmashaur ikupitia Mfumowa O&OD.
• Uratibu na utayarishaji wa Mpango na Bajeti ya kilamwaka ya Halmashauri.
• Kusimamia uandaaji w amipangokazi (Action Plans) ya bajeti za kilamwaka na kuziwasilisha katika ngaz ihusika..
• Kuratibu uandaaji wamaandiko ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
• Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN)
• Kuratibu maandalizi ya Sera na Mpango Mkakati wa Halmashauri
• Kuratibu uandaaji wa taarifa mbalimbali za Halmashauri pamoja na taarifa za utekelezaji wa maagizo kutoka mamlaka za juu za serikali
Sehemuya Usimamizi, Ufuatiliaji naTathmini ya miradi ya maendeleo.
Majukumu ya sehemu hii yapo kamaifuatavyo:-
• Kuratibu uandaaji wa taarifa za Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya 2015 - 2020
• Kufuatilia utekelezaji halisi na matumizi ya fedha zamiradi ya maendeleo.
• Kuratibu miradi ya jumuiya za wananchi na taasisi nyinginezo za ndani na nje ikiwemo miradi ya wahisani
• Kuratibu utekelezaji wa Mipango ya mudamrefu, kati na mfupi ikiwepo Ilani ya Uchaguzi na uandaaji wa taarifa za utekelezaji wa mipango hiyo
• Kuratibu utekelezaji wa mipango shirikishi.
• Kuandaa taarifa za Miradi ya maendeleo ya Manispaa kwa vipindi mbalimbali na kuziwasilisha kwenye mamla kahusika.
• Kuandaa mapitio ya bajeti ya kila mwaka baada ya kipindi cha nusu mwaka
• Kuandaa mapendekezo ya kubadili matumizi ya vifungu vya bajeti ya maendeleo kila inapobidi.
• Kuandaa taarifa za matukio ya kila wiki na kuiwasilisha ngazi ya mkoa.
Sehemuya Uwekezaji.
Sehemu hii hushughulikia mipango ya uwekezaji katika Halmashauri ya Manispaa kwa kufanya yafuatayo:-
1. Kuratibu na kusimamia maandalizi ya mipango ya uwekezaji ya Halmashauri.
2. Kuratibu utekelezaji na uandaaji wa taarifa za mipango ya uwekezaji
Sehemuya Utafiti naTakwimu.
Sehemu hii hushughulikia masuala yanayohusu takwimu mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kuratibu shughuli za utafiti kama ifuatavyo:-
• Kuratibu na kusimamia benki ya Takwimu ya Halmashauri.
• Kuhuisha na kuboresha Takwimu za Kiuchumi na Kijamii (Profile) za Halmashauri.
• Kuratibu na kuhifadhi takwimu za Idadi ya watu za Halmashauri kwa kutumia rejista za wakazi wa Mitaa.
• Kuratibu na kutathmini utekelezaji wa Mpango mkakati wa Halmashauri 2016/17 -2021/22
• Kuratibu zoezi la Sensa ya Watuna Makazi.
• Kuandaa taarifa za utatuzi wa kero na malalamiko kila wiki na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Mkoa
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa