Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mheshimiwa Dalmia Mikaya, ameendelea na ziara yake aliyoipa jina la “Kijiwe kwa Kijiwe” katika mitaa ya Buyuni, Kizitohuonjwa na Minondo(cheka).
Akizungumza na wananchi wa maeneo hayo, Mheshimiwa Mikaya amesema ziara hiyo inalenga kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi na kushirikiana nao katika kuyapatia suluhisho la pamoja.
Aidha, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi mkuu, akibainisha kuwa ni nafasi muhimu ya kidemokrasia ya kuchagua viongozi watakaosimamia maendeleo yao ya kila siku.
“Ni wajibu wetu kutumia haki ya kikatiba ya kupiga kura. Nawaomba wananchi wote tujitokeze kwa wingi ili kuchagua viongozi bora watakaotusaidia kutatua changamoto zetu,” amesema.
Mheshimiwa Mikaya pia amesisitiza ushirikiano na mshikimano wa kijamii, huku akiahidi kuwa serikali ya wilaya itaendelea kushirikiana kwa karibu na wananchi na wadau mbalimbali kuhakikisha changamoto za huduma za jamii zinatatuliwa kwa wakati.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa