• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Livestock na Fisheries
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Sekondary
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Utumishi na Utawala
      • Maji
      • Mipango Mija na Maendeleo ya Ardhi
      • Afya
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Elimu
    • Maji
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba za Vikao
      • Vikao vya Waheshimiwa
      • Kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi ya Sasa
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Umma
    • Picha za Video
    • Hotuba Mbalimbali
    • Picha

“Wauzaji wa maji kigamboni msibeze juhudi zinazofanywa na serikali kuleta maji ya uhakika Kigamboni"

Posted on: February 14th, 2021


Ni kauli ya makamu wa Rais Mhe. Samia Hassan Suluhu alipokuwa akizungumza na wananchi leo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa tanki la maji  linalojengwa Kisarawe II   Wilayani Kigamboni linalohusisha visima 12 na uwezo wa  kuhifadhi maji lita milioni 15 linalojengwa  kwa kutumia fedha za ndani za DAWASA kiasi cha Bilioni 23.

Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali imejitoa kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji  kwa kutumia gharama kubwa  kujenga miundombinu ya maji ili kustawisha afya na maendeleo ya wananchi, Hivyo wananchi wa Kigamboni wanapaswa kuilinda miundombinu hiyo wakati wa utekelezaji wa mradi na hata baada ya kukamilika ili lengo lililokusudiwa liweze kukamilika.

“ Wapo wananchi ambao walichimba visima vya maji na kusambaza kwa wananchi wengine kwa lengo la kuuza , Serikali inapoleta maji ya gharama nafuu wauza maji hao wanabeza ,hii haipendezi  naomba wauza maji msituharibie Siasa nguvu iliyoweka Serikali kutatua changamoto ya maji ni kubwa”

Ameongeza kwa kuwataka Watendaji wa Mitaa kuunda kamati za maji zitakazokuwa na jukumu la kulinda miundombinu ya maji iliyopo katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kusimamia changamoto ya kubambikiwa kwa gharama za bili ya maji wanazopata wananchi kutoka DAWASA.

Mhe. Samia amesema kuwa anaimani hadi kufikia Desemba tatizo la maji Dar es Salaam litakuwa limekwisha nakuwataka Wizara ya Maji kumaliza tatizo la maji  kwa kukamilisha miradi inayojengwa nchi nzima isiwe kwa Dar es Salaam pekee ili lengo la Serikali la hadi kufikia 2025 utatuzi wa changamoto ya upatikanaji wa maji nchini liwe limekamilika.

Aidha Mhe. Samia ameitaka kampuni inayotekeleza ujenzi wa mradi wa maji Kisarawe II  Advent Construction Limited kukamilisha  mradi kwa wakati na kwa viwango  vinavyoptakiwa ili wananchi waweze kunufaika na mradi huo .

Mradi wa ujenzi wa Tanki la maji linalojengwa kisarawe II unatarajiwa kumalizika November na unahusisha visima 12 ambapo hadi sasa visima 7 tayari vinafanya kazi


Ujenzi wa tanki la maji ukiwa katika hatua za awali

Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Cpriyan Luhimija akielezea namna mradi huo utakavyonufaisha wakakzi wa kigamboni na maeneo ya Jirani kama Kongoe na Mbagala kwa Makamu wa Rais.



Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Cpriyan Luhimija akitolea ufafanuzi hatua ya ujenzi wa tanki hilo na namna walivyojipanga kulikamilisha kwa wakati.

Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu akiwa anazungumza na Waizri wa Maji Juma Aweso mara baada ya kukagua mradi

 

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Sara Msafiri akizungumzia kwa uchache namna Wilaya ilivyo na matarajio na mradi huo na utakavyonufaisha wakazi wa Kigamboni.

Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Cpriyan Luhimija akitolea ufafanuzi jinsi DAWASA ilivyojipanga kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji  Kigamboni na  Dar es Salaam kwa ujumla.


Makamu wa Rais na Viongozi wengine wakiendelea kupokea ufafanuzi jinsi DAWASA ilivyojipanga kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji Dar es Salaam.

Matangazo

  • TANGAZO LA USAFI KWA WAMILIKI WA ARDHI NA MAJENGO MBALIMBALI KIGAMBONI February 15, 2021
  • TANGAZO LA UCHAGUZI WA WAJUMBE WA BODI YA AFYA YA HALMASHAURI NA KAMATI ZA AFYA ZA VITUO MANISPAA YA KIGAMBONI. December 03, 2020
  • MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE ZA SEKONDARI MANISPAA YA KIGAMBONI December 16, 2020
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • “Wauzaji wa maji kigamboni msibeze juhudi zinazofanywa na serikali kuleta maji ya uhakika Kigamboni"

    February 14, 2021
  • Madiwani waahidi Wataalamu wa Manispaa kushirikiana katika shughuli za maendeleo.

    January 28, 2021
  • LEAT kushirikiana na Serikali kutatua changamoto za kimazingiraa kwa ustawi wa afya za wananchi

    January 20, 2021
  • Wajumbe wa Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango wapongeza Menejiment kwa usimamizi mzuri wa miradi.

    January 19, 2021
  • Angalia Zote

Video

Makala ya Miradi ya Maendeleo Kigamboni Manispaa
Video zingine

Kurasa za karibu

  • Municipal councilors
  • Kigamboni Municipal History
  • Investment Opportunities
  • Fomu ya Maombi ya Kiwanja
  • Huduma za Afya na Orodha ya Vituo vya kutolea Huduma za Afya

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni

    Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam

    Simu: +255222928468

    Simu ya Mkononi: +255222928468

    Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa