Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw. Erasto Kiwale amewaasa watumishi wa manispaa ya Kigamboni kuzingatia kutoa huduma bora kwa wateja wanaofika Halmashauri kupata huduma.
Bw. Kiwale ameyasema hayo leo Juni 13, 2025 katika Ofisi za Mkurugenzi wakati akikabidhi vyeti kwa watumishi wa Manispaa ya Kigamboni waliopatiwa mafunzo ya huduma kwa wateja wa ndani na nje wa Taasisi.
“Sifa nzuri ya Taasisi inategemea na mtu mmoja anavyompokea na kumhudumia mteja, ukumhudumia vizuri anakwenda kuisemea vizuri Taasisi, hivyo tuzingatie sana namna ambavyo tuwahudumia wateja wetu kama ilivyo kwenye Mkataba wa Huduma kwa Wateja, kuanzia lugha pamoja na ukarimu, tukizingatia hayo mahusiano yetu na tunaowahudumia yataimarika” amesema Bw. Kiwale.
Aidha Bw. Kiwale imeipongeza idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kuendelea kwa usimamizi mzuri na miongozo inayotolewa kwa watumishi hao wanaokutana na wateja kabla ya kwenda kupata huduma mbalimbali na kusisitiza elimu hiyo iwafikie watumishi wote.
Akitoa neno la Shukrani Bi. Herieth Gwimo, Mwandishi mwendesha Ofisi ambaye ni miongoni mwa watumishi waliopata mafunzo ameshukuru kwa fursa ya elimu waliyoipata huku akielezea namna elimu hiyo ilivyowabadilisha katika utendaji kazi.
Ikiwa ni muendelezo wa kuboresha utoaji wa huduma na ili kuongeza ufanisi Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imewapeleka watumishi Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kuwanoa eneo la huduma kwa wateja ili kuhakikisha inatoa huduma kasi na Ubora wa hali ya juu
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa