Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka wananchi wa Manispaa ya Kigamboni kutoa ushirikiano kwa wakandarasi wanaojenga barabara ndani ya Manispaa hiyo, huku akiwaasa kuwa walinzi wa vifaa vinavyotumika wakati wa ujenzi pamoja na miundombinu mbalimbali ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Rais Mhe Dkt Hussain Ali Mwinyi ametoa wito huo leo aprili 25. 2025 katika hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami inayojengwa kutoka Kibada, Mwasonga hadi Kimbiji yenye urefu wa KM 41 kwa gharama ya Tsh Bil 83, ikiwa ni kuadhimisha miaka 61 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar.
Aidha amemtaka mkandarasi kutoka Estim construction Limited kufanya kazi kwa bidii na kwa weledi ili barabara hiyo iweze kukamiljka kwa wakati na kwa kiwango madhubuti huku akimtaka kuzingatia masharti ya Mkataba katika kutekeleza mradi huo.
Kwa upande mwingine mtendaji mkuu wa wakala wa barabara Tanzania (TANROAD) Eng. Mohamed Besta amesema mradi wa ujenzi wa barabara ya Kibada - Mwasonga umefikia asilimia 38 na umetoa ajira kwa Wananchi wapatao 331.
Aidha amesema mradi unatarajia kukamilika tarehe 09/12/2025 na utachangia ukuaji wa uchumi ndani na nje ya Manispaa ya Kigamboni kupitia viwanda na ajira. kwani eneo hilo limetengwa mahususi kwaajili ya uwekezaji.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa