UTANGULIZI:
Idara ya Ujenzi imegawanyika katika sehemu nne kama ifuatavyo:
(i) Barabara
(ii) Usanifu Majengo
(iii) Majengo
(iv) Mitambo
MAJUKUMU:
• Ukadiriaji wa mahitaji ya ujenzi wa barabara na majengo
• Kusimamia miradi ya ujenzi wa barabara na majengo ya kiofisi/kihuduma (kama Ofisi za Kata, mashule, hospitali, n.k).
• Kusimamia maendeleo ya ujenzi mjini kwa ushirikiano na Mipango miji kwa mujibu wa ‘The Local Government Urban Authorities Act (Cap.288) na ‘Urban planning Act, 2007’’
• Kuratibu shughuli za uwekaji wa mabango na minara ya mawasiliano kwa mujibu wa ‘’By Laws’’.
• Kufanya tathmini ya ubora wa magari ya Manispaa na kuyafanyia matengenezo magari yote ya Manispaa
BARABARA
Idara ya Ujenzi inasimamia mtandao wa barabara zenye jumla ya urefu wa km. 489.10. Kati ya hizo km 113.9 ni barabara za changarawe na km. 375.2 ni barabara za udongo. Pia wakala wa barabara (TANROADS) inasimamia mtandao wa barabara zenye jumla ya km 114.5. Kati ya hizo km 46 ni barabara za lami na km 68.5 ni changarawe.
USANIFU MAJENGO
Ufuatao ni utaratibu wa kutoa vibali (taratibu za kupata kibali cha ujenzi idara ya ujenzi)
1. KIBALI CHA UJENZI
Kulingana na sheria ya ujenzi wa majengo mijini si ruhusa kwa mtu yeyote kujenga au kuanza jengo jipya bila ya:
(i) Kutuma maombi kwa mamlaka ya mji
(ii) Kuwasilisha michoro ya jengo na kumbu kumbu husika.
(iii) Kupata kibali kwa maandishi 'kinachoitwa “kibali cha ujenzi.”
2. KIBALI CHA AWALI (Planning consent)
Inashauriwa kupata kibali cha awali kabla ya kuomba kibali cha ujenzi. Hivyo muendelezaji anatakiwa aandae mchoro wa awali (outline plan) kwa utaratibu unaotakiwa ukionyesha aina ya ujenzi utakao kusudia kufanya ili aweze kupata ridhaa ya kuendelea na hatua za kuanda michoro ya mwisho.
Faida:
• Kuokoa muda wa gharama iwapo michoro ya mwisho itaonekana kuwa na dosari za kitaalamu ambazo zitahitaji kufanyiwa marekebisho.
• Kuwa na uhakika kuhusu mahitaji muhimu ya kuzingatiwa wakati michoro inaandaliwa.
3. JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI YA KIBALI CHA UJENZI
Baada ya michoro kukamilika iwasilishwe ikiwa kwenye majalada kwa namna ambayo inawezekana kufunguliwa na kusomeka. Michoro hiyo iwasilishwe kwa utaratibu ufuatao
• Seti tatu za michoro ya jengo (architectural drawing)
• Seri mbili za michoro ya vyuma (Structural drawing) kwa michoro ya ghorofa
4. MICHORO ILIYOANDALIWA IONYESHE NINI ?
Michoro iliyoandaliwa inatakiwa ionyeshe mambo yafuatayo:
• Namna jengo litakavyokuwa (plans sections, elevation, foundation and roof plan).
• Namba na eneo la kiwanja kilipo.
• Jina la mmiliki ardhi inayohusika.
• Jina la mchoraji ujenzi na anwani.
• Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba.
• Ujazo wa kiwanja (Plot coverage).
• Uwezo (Plot ratio)
• Matumizi yanayo kusudiwa.
• Idadi ya maegesho yatakayo kuwepo.
• Umbali wa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja (atbacks)
• Mfumo wa kutoa maji taka hadi kwenye mashimo
5. VIAMBATANISHO
• Fomu za maombi zilizo jazwa kwa usahihi
• Hati ya mmiliki wa kiwanja au barua ya toleo
• Kumbu kumbu zingine zinazohusu kiwanja hicho kama hati ya mauzo, makabidhiano n.k
• Nakala za risiti ya kodi ya kiwanja ya sasa.
• Mabadiliko ya matumizi ya ardhi kama muombaji amebadilisha matumizi ya awali
6. HATUA ZINAZOFUATA KATIKA KUSHUGHULIKIA MAOMBI YA KIBALI
Zifuatazo ni hatua zinazofuatwa wakati wa kuchunguza michoro hiyo:
• Uhakiki wa miliki
• Kukaguliwa usanifu wa michoro.
• Kukagua kiwanja kinachokusudiwa kuendelezwa.
• Uchunguzi wa matumizi ya jengo na uwiano.
• Uchunguzi wa maofisa wa afya.
• Uchunguzi wa mipango ya uondoaji wa maji taka.
• Uchunguzi wa tahadhari za moto.
• Uchunguzi wa uimara wa jengo.
• Kuwasilisha kwenye kikao cha mipango miji na mazingira baada ya kukamilisha taratibu zote.
• Hatimaye kuandika na kutoa kibali
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa