kata ya Tungi iko Kaskazini - magharibi mwa Wilaya ya Kigamboni inapakana na Kata ya Kigamboni upande kaskazini Magharibi,Kusini inapakana na kata ya Vijibweni, Mashariki inapakana na Kata ya Mjimwema.
Utawala;
Ofisi ya Kata ipo Mtaa wa Tungi
Idadi ya Watu
Kata ya Tungi in jumla ya Wakazi 29,988. Wanaume 13,694 Wanawake 14,294
Diwani
Diwani wa kata hii ni Mh. Ernest Ndamo Mafimbo na Amina Ally Yakubu Diwani wa Viti Maalumu.
Shughuli za kiuchumi
Kata ya Tungi inashughuli mbalimbali za kiuchumi na watu wengi wamejiajiri katika biashara hasa Mtaa wa tungi na Magogoni.
Daraja la Nyerere maarufu kama Kigamboni linaptokana katika kata hii katika mtaa wa wa Mungano. Mtaa huu una hifadhi (Matanki) ya Mafuta, Kampuni nyingi zimewekeza katika mtaa huu. Kuna Hospitali ya jeshi na Shule ya Sekondari ya jeshi.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa