HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI
TAARIFA FUPI YA MPANGO WA MAENDELEO KWA USTAWI WA TAIFA NA MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO-19 KATIKA TAWALA ZA MIKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA MWAKA WA FEDHA 2021/2022
UTANGULIZI
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ni moja kati ya Manispaa 5 zinazounda Jiji la Dar es Salaam, ambapo upande wa Kusini mwa Jiji hilo inapakana na Wilaya ya Mkuranga na Mashariki inapakana na Bahari ya Hindi (fukwe yenye urefu wa kilomita 60)
Awali Kigamboni ilikuwa sehemu ya Manispaa ya Temeke mpaka mwaka 2015 ilipotangazwa rasmi kupitia gazeti la Serikali lenye GN No. 462 kuwa Manispaa kamili inayojitegemea. Hata hivyo Kigamboni ilianza rasmi kutekeleza majukumu yake kama Manispaa mnamo Septemba 2016.
Kijiografia KIgamboni ina ukubwa wa kilomita za mraba 577.9 sawa na hekta 57.786 ambapo kiutawala ina Tarafa 3 yaani Kigamboni, Somangila, na Pembamnazi, Kata 9 na mitaa 67. Pia ina jumla ya Madiwani 13 na Mbunge mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Shughuli kuu za uchumi ambazo wananchi wake wanategemea ni Kilimo, Uvuvi, Ufugaji, Biashara na Utalii.
UTEKELEZAJI WA MIRADI
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kupambana na ugonjwa wa UVIKO-19 zimewezesha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupata mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Kimarekani Milioni 567 sawa na shilingi trilioni 1.3 za Tanzania, kutoka Shirika la fedha la Kimataifa (IMF) kwa ajili ya kampeni ya maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 ili kuchangia kufufua uchumi kwa sekta zilizopata athari za kiuchumi kutokana na madhara ya UVIKO-19.
MAPOKEZI YA FEDHA
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imeidhinishiwa kupokea jumla ya shilingi 1,260,000,000.00, kwa sekta ya Elimu ya Msingi, ni shilingi 160,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 4 katika vituo shikizi na bweni 1, kwa sekta ya afya ya msingi ni shilingi 420,000,000.00 kwa ajili ya ununuzi wa mashine ya miyonzi (X-ray) na kwa sekta ya Elimu ya Sekondari ni shilingi 680,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 34. Tarehe 20/10/2021 tumeingiziwa Jumla ya Tsh. 840,000,000.00 katika akaunti ya Manispaa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 38 na bweni 1.
HALI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI
Ktika uekelezaji Manispaa ya Kigamboni ina Jumla ya maeneo ya kutekeleza miradi hii 10 yanayopatikana katika kata 6.
Kwa taarifa zaidi bofya linki https://kigambonimc.go.tz/gallery
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa