TAARIFA YA KIKUNDI CHA WACHAPATOYO
Kikundi cha Wachapatoyo kipo katika mtaa wa Mdoe kata ya Somangila, Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni. Kikundi cha Wachapatoyo ni kikundi cha ujasiliamali ambacho kinachojishughulisha na usafirishaji wa mizigo kwa kutukia Usafiri wa Gutta.
Kikundi kilianzishwa mnamo 15/03/2021 kikiwa na Wanachama wakiume watano (5) ambao ndio waliopo hadi sasa. Kikundi kilisajiliwa rasmi kisheria kama Kikundi cha Vijana tarehe 30/11/2022, kwa namba ya usajili DAR/KIG/VIJ/2022/0460 na Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.
Kikundi hiki kilianza na mtaji wa shilingi 1,000,000 ikiwa ni pesa zilizopatikana baada ya kuchanga kiasi cha shilingi 200,000 kwa kila Mwanakikundi na tarehe 10/03/2023 tulifanikiwa kupata mkopo wa asilia 10 unaotolewa na Manispaa ya Kigamboni (asilimia 4 za vijana) kwa ajili ya ununuzi wa maguta 5 yenye thamani ya shilingi 43,750,000 na kuendelea kurejesha kulingana na muongozo na mkataba unavyoelekeza, ambapo kwa kila mwezi tunalipa kiasi cha shilingi 1,900,000 mpaka sasa tumeweza kurejesha kiasi cha shilingi 20,000,000 na kubakisha na deni la kiasi cha shilingi 23,750,000 ambacho unatakiwa kumalizika Mwaka 2025 mwezi wa tano (05).
Mradi huu umetunufaisha kama ifuatavyo;
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa