Katika kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinajitengenezea mazingira ya kujitegemea kifedha kupitia fursa za masoko ya mitaji na uwekezaji, Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ni miongoni mwa Halmashauri iliyofanikiwa kupata mradi mkakati mmoja wa Ujenzi wa Soko la Kisasa la Kibada linalojengwa kwenye Kata ya Kibada.
Mradi huu upo kwenye hatua za ukamilishaji na utagharimu kiasi cha Tsh.6.6 Bilioni hadi kukamilika,Jengo hili la kisasa litajengwa na Mkandarasi Mwananchi Engineering and Construction Company Ltd (MECCO) huku Mhandisi Mshauri akiwa ni Bureau for Industrial Cooperation (BICO).
Ujenzi umeanza tarehe 16/08/2019 ambapo hadi kukamilika kwa mradi mbali na kuongeza pato la Manispaa kwa kukusanya Kodi lakini pia utawezesha;
Mradi wa soko utakapokamilika utapunguza adha ya umbali na gharama ya usafiri kwa wananchi waliokuwa wakifuata huduma za bidhaa za soko nje ya Wilaya,
Wafanyabiashara zaidi ya 320 watanufaika na mradi huu kwa kuboreshewa mazingira mazuri ya kufanya biashara,
Bidhaa za sokoni kama vile matunda mbogamboga zitashuka kwa kuwa zitakuwa zikipatikana karibu na kwa urahisi .
Muonekano wa mradi kwa sasa
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa