Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Mikaya Tumaini Dalmia amewataka watendaji wa Kata na Mitaa ndani ya Manispaa ya Kigamboni kufuata taratibu na sheria za Manunuzi wakati wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili iweze kuendana na thamani ya fedha.
DC Mikaya ametoa agizo hilo leo Julai 15. 2025 katika kikao chake na watendaji hao kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi yake kwa lengo la kujadili namna bora ya kuendesha shughuli za Serikali.
Aidha amewataka kutunza vizuri nyaraka zinazoandaliwa wakati wa utekelezaji wa miradi ili kuepuka hoja zisizo za lazima.
Pia amewataka kuwahamasisha wananchi kufanya usafi kila wakati na sio kusubiri hadi kampeni za usafi za mwisho wa mwezi zinazoandaliwa na kufanywa na Serikali.
Kwa upande mwingine amewataka watendaji hao kufuata miongozo taratibu na kanuni za utumishi wa umma wakati wa kuwahudumia wananchi.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa