WALIMU WAJENGEWA UWEZO KUHUSU MFUMO WA MANUNUZI YA SERIKALI KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA BOOST
Mratibu wa Mradi, Bi Hellen Peter, amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025, shule mbalimbali katika Wilaya ya Kigamboni zimepokea jumla ya shilingi milioni 809.7 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa madarasa 19 na matundu ya vyoo 49 kupitia mradi wa BOOST.
Akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu kuhusu matumizi ya Mfumo wa Manunuzi ya Serikali kwa Njia ya Kielektroniki (NEST), Bi Hellen alieleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha walimu kuelewa na kutumia mfumo huo ipasavyo ili kutekeleza miradi ya serikali kwa ufanisi, uwazi na uadilifu.
Kwa upande wake, Afisa Manunuzi kutoka Idara ya Elimu Msingi Wilaya ya Kigamboni, Bw. Stanley Kalalu, alifafanua kuwa mafunzo hayo yalihusisha maeneo muhimu kama vile mifumo ya manunuzi, ununuzi na upokeaji wa vifaa, utoaji wa vifaa, uundaji wa kamati za ujenzi, pamoja na usimamizi wa nyaraka mbalimbali za manunuzi.
Mafunzo haya yanatarajiwa kuongeza ufanisi katika usimamizi wa miradi ya maendeleo ya elimu kwa kuhakikisha fedha za serikali zinatumika kama ilivyokusudiwa.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa