Kituo cha Afya Tundwi Songani kinajengwa katika Kata ya Pembamnazi, ambayo ni miongoni mwa Kata 9 zinazounda Wilaya ya Kigamboni. Kituo hiki kipo umbali wa kilometa 52 kutoka Ofisi ya Manispaa ya Kigamboni. Lengo la kujenga Kituo hiki ni kuwapunguzia wananchi kero ya kutembea umbali mrefu kufata huduma za afya katika Kata na Wilaya Jirani ya Mkuranga.
Kituo cha Afya Tundwi Songani kilipokea jumla ya Tsh. 500,000,000.00 kutoka Serikali Kuu. Mradi huu ulihusisha nguvu za wananchi kwa kutoa eneo la Ekari 9 lenye thamani ya Tsh. 54,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya ili kusogeza na kuboresha huduma za afya kwa wakazi wa eneo hilo na walioko karibu na Kata ya Pembamnazi.
Utekelezaji wa Mradi huu wa Kituo cha Afya Tundwi Songani unahusisha ujenzi wa majengo manne (4) ambayo ni; Jengo la wagonjwa wa nje (OPD), Jengo la Wodi ya wazazi, Jengo la Upasuaji Pamoja na Maabara. Utekelezaji ulianza mwezi Oktoba, 2021 na unatarajiwa kukamilika mwezi Mei, 2022, kwa kutumia utaratibu wa ‘Force Account’. Hadi kufikia sasa mradi upo asilimia 85.5% ya utekelezaji kwa majengo yote na jumla ya kiasi cha Tsh. 464,553,031.85 zimetumika. Hatua ya ujenzi iliyofikiwa ni uwekaji wa skimming katika majengo yote.
Mradi utakapokamilika unatarajiwa kuhudumia jumla ya wakazi 8500, waliopo katika Kata ya Pembamnazi, Kata jirani na wakazi kutoka Wilaya ya Mkuranga. Aidha miongoni mwa faida zitakazopatikana ni pamoja na kusogeza huduma za afya karibu na wakazi wa eneo hilo, kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi kwa kina mama wajawazito, vifo vya watoto wachanga na vifo vya watoto chini ya miaka mitano.
Jengo la maabara.
Jengo la wazazi
Muonekano wa majengo matatu kwa mbali
Kituomcha Afya tundwi songani kiliwekwa jiwe la Msingi na Mkimbiza Mwenge kitaifa wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mei 13, 2022
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa