• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Care Values
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu ya awali na Msingi
      • Kilima mifugo na umwagiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Sekondary
      • Mipango na uratibu
      • Utawala na usimamizi wa Rasilimali watu
      • Viwanda biashara na Uwekezaji
      • Miundombinu ,Vijijini na Mjini
      • Huduma za Afya, Ustawi wa jamii na Lishe
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
        • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa ndani
      • Usimamazi wa Manunuzi
      • Maliasili na uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na uhasibu
      • Usimamizi na usafi wa Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Elimu
    • Utumishi
    • Huhuma za Kisheria
    • Usafi wa mazingira na udhibiti wa taka ngumu
    • Michezo na Sanaa
  • Madiwani
    • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipangomji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
      • Huduma za jamii
    • Ratiba za Vikao
      • Vikao vya Waheshimiwa
      • Kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
      • Miradi ya Sasa
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Picha
    • Hotuba
    • Gazeti la Mtandaoni
    • Vipeperushi
  • Mifumo

ZIARA YA NAIBU KATIBU MKUU OR-TAMISEMI (ELIMU)

Posted on: November 16th, 2022

NAIBU KATIBU MKUU OR-TAMISEMI (ELIMU) AFANYA ZIARA MANISPAA YA KIGAMBONI,MPANGO UBORESHAJI MIUNDOMBINU SHULE ZA MSINGI WAPAMBA MOTO


Leo hii 16/11/2022 Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI ndg.Ramadhani Kailima amefanya ziara katika Manispaa ya Kigamboni kwa nia ya kukagua miradi pamoja na kutembelea shule za msingi zenye changamoto za miundo mbinu.


Akiwa katika ziara hii Ndg.Kailima amepitia shule takribani tano na kufanya ukaguzi wa miundo mbinu inayohitaji ukarabati na mapungufu upande wa madawati,matundu ya vyoo,ofisi za walimu.Shule zilizotembelewa ni AboudJumbe,Kidete,Kibugumo, Mjimwema na Kisota.


Aidha katika ziara hiyo ndg.Kailima amejionea uchakavu wa madarasa mbalimbali yanayohitaji kukarabatiwa,upungufu matundu ya vyoo,upungufu wa madawati na madarasa na kujazana kwa wanafunzi katika madarasa kutokana na kutotosheleza.


Akizungumza amesema mapungufu yote aliyoyashuhudia ameyachukua kwa ajili ya kwenda kuyawasilisha ili yafanyiwe kazi kupitia Mpango huu wa serikali  ya awamu ya sita ambapo sasa inaenda kuboresha miundo mbinu ya shule za msingi kama ilivyofanya kwa shule za sekondari.

     "Tunamshukuru Mh.Rais wetu      kwa kuja na mpango huu ambao sasa unaenda kutatua changamoto kwa upande wa shule za Msingi."alisema ndg.Kailima


Pamoja na ukaguzi wa miundo mbinu Naibu Katibu Mkuu amekagua pia baadhi ya madarasa ya kidato cha kwanza yanayojengwa hivi sasa kupitia fedha za kapu la mama ambapo kwa Manispaa ya Kigamboni ilipata shs.Mil.200 kutekeleza ujenzi wa madarasa 10.


Pamoja na hayo amegusia suala la udhalilishaji wa watoto kushika kasi hivyo amewataka walimu kuwa karibu na wanafunzi ili kuyajua wanayopitia kwa upande huo na ameshauri kuwepo kwa Dawati linaloshughulika na maswala ya udhalilishaji wa wanafunzi.Pia suala la madawa ya kulevya halikuwa nyuma kwani amewataka walimu kuwa makini na wauzaji wa biskuti na pipi wanaofika mashuleni kuuzia watoto kwani umezuka mtindo wa kuweka madawa ya kulevya katika pipi na biskuti jambo linalopelekea watoto kujiingiza katika madawa ya kulevya bila kujijua.


Ziara hii ni kufuatia mpango huo wa uboreshaji wa miundombinu kwa shule za msingi ambao serikali ya awamu ya sita ya Mh.Samia Suluhu Hassan imeamua kuutekeleza ili kuboresha miundo mbinu ya shule za msingi,hivyo unafanyika ukaguzi katika mashule kubaini maeneo yote yanayohitaji kuboreshwa, aidha ni utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi katika kuwaletea wananchi maendeleo.


Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

Matangazo

  • Tangazo la Frem za Biashara, Soko la Kibada February 26, 2025
  • Tangazo la kuitwa kwenye usaili nafasi ya mwendesha mashine ya Bayometriki na Mwandishi msaidizi February 24, 2025
  • Tangazo la uteuzi wa wajumbe wa bodi ya Afya March 26, 2025
  • Tangazo la kuitwa kazini nafasi ya mwendesha mashine ya Bayometriki na Mwandishi msaidizi March 12, 2025
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHE. DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AMEWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA KIBADA - MWASONGA

    April 25, 2025
  • MANISPAA YA KIGAMBONI IMEPOKEA VITI MWENDO 35 NYENYE THAMANI YA TSH MIL 8

    April 08, 2025
  • MKANDARASI TOKA SUMA JKT ATAKIWA KUANZA MAPEMA MAANDALIZI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA TUNGI

    April 08, 2025
  • Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele amefanya ziara ndani ya Manispaa ya Kigamboni

    March 22, 2025
  • Angalia Zote

Video

Makala maalumu ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Kigamboni
Video zingine

Kurasa za karibu

  • Municipal councilors
  • Kigamboni Municipal History
  • Investment Opportunities
  • Fomu ya Maombi ya Kiwanja
  • Huduma za Afya na Orodha ya Vituo vya kutolea Huduma za Afya

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni

    Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam

    Simu: +255222928468

    Simu ya Mkononi: +255222928468

    Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa