Mhe Ernest Mafimbo ametoa agizo hilo leo Aprili 8. 2025 katika makabidhiano ya eneo la ujenzi wa mradi wa kituo cha Afya cha Tungi yaliyofanyika katika Mtaa wa Magogoni, Kata ya Tungi, Manispaa ya Kigamboni.
Aidha amesema kwa muda mrefu wananchi wa Kata ya Tungi wamekuwa wakifuata huduma ya Afya katika kata za jirani hivyo kukamilika kwa kituo hicho kutawapunguzia umbali wa kufuata huduma ya Afya katika maeneo ya jirani.
Kwa upande mwingine amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. DKT Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha kwaajili ya ujenzi wa vituo vya Afya ndani ya Manispaa ya Kigamboni.
Akizungunza mara baada ya kukabidhiwa eneo hilo Mkandarasi wa Suma JKT Letenenti J. Mkamba amawataka wananchi wa eneo la jirani kuchangamkia fursa za ajira zitakazotokana na mradi huo ili waweze kujipatia kipato.
Kituo cha Afya cha Tungi kinatajiwa kujengwa kwa njia ya gorofa na kitagharimu kiasi cha Tsh Bil 7 ikiwa ni fedha ya makusanyo ya mapto ya ndani.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa