Leo Aprili 08. 2025 Diwani wa Kata ya Tungi na Mstahiki meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Ernest Mafimbo amepokea msaada wa viti mwendo 35 vyenye thamani ya Tsh Mil 8 kutoka kwa taasisi ya Qatar ikiwa ni mchango wao katika kuadhimisha wiki ya afya kitaifa.
Akizungunza mara baada ya kupokea viti mwendo hivyo Mhe. Ernest Mafimbo amewashukuru wadau mbalimbali ndani ya Manispaa kwa michango yao ya vifaa tiba katika kuboresha utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi wa Kigamboni.
Aidha katika maadhimisho hayo amawataka wananchi wa Manispaa kuanzisha utaratibu wa kucheki afya zao mara kwa mara ili kuepuka magonjwa yasiyoambukizwa kama vile saratani kisukari na shinikizo la damu.
Akizungunza wakati wa kupokea viti hivyo mganga mkuu wa Manispaa ya Kigamboni Dkt. Lucus Ngamtwa amesema viti 17 kati ya 35 vitatolewa kwa watoto wenye mahitaji maalumu na viti 18 vitatumika kuwahudumia wagonjwa katika vituo vya afya vya Manispaa
Wiki ya afya imeanza siku ya ijumaa tarehe 04/04/2025 na imekamilika leo 08/04/2025 ambapo huduma mbalimbali za kitabibu zilitolewa na jumla ya wagonjwa 374 walijitokeza na kupatiwa matibabu.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa