Leo Machi 21. 2026 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele amefanya ziara ndani ya Manispaa ya Kigamboni yenye lengo la kujionea namna zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapjga kura linavyoendelea
Aidha katika ziara hiyo jaji Mstaafu amemuagiza Afisa Muandikishaji Jimbo la Kigamboni Bw. Selemani Kateti kuongezeko Mashine za kuandikishia wapiga kura (BVR) katika vituo kutokana na muitikio mkubwa ili wananchi wapate nafasi ya kujiandikisha
“Lengo la kufika ni kuangalia kama kumekuwa na changamoto zozote na namna ambazo mmezikabili changamoto hizo, tumeona muitikio ni wa kutosha hii inachangiwa na mwamko pia wa wakazi wa hapa (Kigamboni), ongezeni zaidi vifaa pamoja na waandikishaji maeneo ambayo tumeona muitikio umekuwa mkubwa zaidi ili kuwezesha zoezi hili kwa ufanisi” amesema Mhe. Mwambegele.
Zoezi la kuandikisha na kuboresha taarifa katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura limeanza Machi 17, 2025 na linatarajiwa kukamilika Machi 23, 2025
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa