Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni inatarajia kutumia zaidi ya bilioni 5 kwaajili ya ujenzi wa makao makuu ya Manispaa yanayojengwa eneo la Gezaulole.
Akitoa taarifa ya mradi kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Bw. David Sukali kwa viongozi wa UVCCM Mkoa waliotembelea kuona hatua mradi iliyofikia mwishoni mwa wiki alisema kuwa, ujenzi upo kwenye hatua za awali ambapo Mkandarasi Tanzania Building Agency(TBA) Bridge ndiye aliyepewa tenda ya ukamilishaji wa jengo hilo.
Aliongeza kuwa jengo hilo linajengwa kwa kutumia gharama kutoka Serikali kuu na fedha za ndani za Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Kaimu Mkurugenzi alieleza kuwa mradi utakapokamilika unatarajiwa kuwa na manufaa kwa watumishi wote wa Manispaa ya kigamboni, wakazi wote na Wilaya jirani za Kigamboni na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ujumla.
Alisema kuwa mradi upo kwenye hatua za awali za utekelezaji “mobilization and site clearance” ambapo fedha zilizotumika mpaka sasa ni Tshilingi.500,000,000/=.
Mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la Manispaa ya Kigamboni ulianza Januari 2018 na unatarajiwa kumalizika Agosti 2018
Viongozi wa UVCCM Mkoa walipongeza hatua zilizofikiwa na kusisitiza Mkandarasi kufanya kazi kwa juhudi ili kukamilisha mradi kwa wakati uliopangwa ili wananchi waweze kupata huduma bora.
viongozi wa UVCCM wakifatilia kwa makini taarifa ya maradi ya ujenzi wa makao makuu.
Kaimu Mkurugenzi Bw.David Sukali akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa makao makuu eneo la Gezaulole.
kazi ikiendelea ikiwa ni hatua za awali
Viongozi wakisaidiana na mafundi kuingiza nondo ndani ya shimo.
Viongozi wakiendelea kushiriki nguvu kazi.
Viongozi wakipata taarifa fupi eneo la mradi.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa