MSAADA WA VIFAA TIBA KUTOKA UJERUMANI KWA HOSPITALI ZA WILAYA, KIGAMBONI YANUFAIKA
Leo 22/7/2022 hospitali ya Wilaya ya Kigamboni imepokea vifaa tiba ( vitanda 108 na kabati zake 38 pamoja na vyuma 161 vya kunin'ginizia miguu na dripu ) mara baada ya uzinduzi wa vifaa hivyo uliofanywa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.Amos Makalla ambae alikuwa ni mgeni rasmi aliezindua vifaa hivyo na kukabidhi Kwa Wilaya 5 za mkoa wa Dar es salaam.
Akiongea katika uzinduzi huo Mkuu wa mkoa amewashukuru wadau hao kutoka Hamburg Germany ambao Wana ushirikiano na Tanzania wa muda tangu mwaka 2007.Pamoja na hayo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kudumisha mahusiano na nchi za nje ambapo katika kipindi chake mahusiano yameimarika na kuinufaisha nchi yetu.Pamoja na hayo ameipongeza Manispaa ya Kigamboni kwa jinsi inavyokua kwa Kasi kutokana na kazi nzuri inayoendelea kufanywa hapa Kigamboni.
Aidha amesema kuwa msaada huo ni wa awamu ya pili ambapo kuna container zingine zitakuja zitakazoleta vifaa tiba vingine vitakavyosambazwa pia kwenye vituo vya afya vinavyoendelea kujengwa.
Mh.Mbunge wa Kigamboni Mh.Ndugulile akiongea katika hafla hiyo amemshukuru Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoinyanyua kigamboni kimaendeleo mbalimbali ikiwepo kuipatia pesa mil 420 za UVICO ,mkopo wa bil.1.5 kwa Manispaa kwa ajili ya kuendelea kuipanga Kigamboni,sekta ya afya ununuzi wa X-ray katika hospitali ya wilaya ambayo ilikuwa kero kubwa.Licha ya hayo amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa namna wilaya kwa utendaji wake na usimamizi na kuifanya Wilaya kwenda kwa Kasi katika maendeleo katika Nyanja mbalimbali.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Almas Nyangasa Kigamboni amewashukuru wadau hao Kwa msaada huo kwani utasaidia kutatua upungufu uliokuwepo,Aidha amemshukuru Rais wa Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuifungua nchi na kupelekea kuongezeka kwa mahusiano baina ya nchi yetu na nchi za nje.Pia amempongeza Mh.Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa jinsi ambavyo amekuwa akitupia jicho katika kila sekta kuhakikisha Dar es salaam inafanya vizuri.
Akiongea Meya Manispaa ya Kigamboni Mh Ernest Mafimbo ameshukuru Kwa kupatikana vifaa hivyo kwani vinaenda kutatua changamoto iliyokuwepo ya uhaba wa vitanda.
Wilaya zingine zilizonufaika ni Ilala,kinondoni,Ubungo na Temeke
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI MANISPAA KIGAMBONI
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa