Maelekezo hayo yametolewa leo na Afisa Utumishi Mkuu Bw. Wenslausi Lindi mwakilishi wa Mkurugenzi kwenye ukumbi wa G5 walipokuwa wakipewa semina elekezi ya masuala mtambuka katika utendaji kazi yaliyohusisha Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa ikiwa na lengo la kutoa uelewa wa pamoja utakaowawezesha kufanya kazi kwa kuzingatia mipaka ya maeneo yao ili kuwezesha wananchi kupata huduma bora.
Aidha wameelekezwa pia kuhakikisha wanasimamia sheria na taratibu za ujenzi na wanakua walinzi wa ujenzi holela kwa kutoa taarifa katika ofisi husika ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa yeyote ataayekiuka utaratibu uliowekwa wenye lengo la kuijenga Kigamboni.
Viongozi hawa wanaokutana na wananchi moja kwa moja leo wameweza kupewa semina kwenye masuala ya uwajibikaji na majukumu yao,sheria ndogondogo na taratibu za uundaji wa mabaraza ya Kata, mfumo wa fursa na vikwazo,utaratibu wa utoaji wa vibali vya ujenzi, suala la ukusanyaji wa mapato, majukumu katika masuala ya kilimo, uboreshaji wa usafi na mazingira na udhibiti wa taka ngumu pamoja na majukumu ya Watendaji wa Kata, Mitaa na Wenyeviti wa Mitaa katika masuala yahusuyo ushirikishwaji , mikopo na mfuko wa TASAF.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria Charles Lawiso akitoa ufafanuzi wa sheria mbalimbali zinazotuongoza Manispaa katika utendaji kazi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Vibali vya Ujenzi Magdalena Malunda akielezea taratibu za upatikanaji wa vibali vya ujenzi.
Baadhi ya Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa wakifatilia mada zinazotolewa
Rajabu Gundumu mchumi akielezea namna ya uibuaji wa fursa katika utekelezaji wa miradi.
Msimamizi wa TASAF kwenye Idara ya Maendeleo ya jamii Bi. Edda Gweba aikielezea wajibu wa wenyeviti wa Mitaa, Wtendaji wa Kata na Mitaa katika kutekeleza mfuko huo.
Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira akielezea wajibu wa kila kiongozi katika kutunza mazingira
Dokta Kadula kutoka idara ya afya akielezea namna bora ya mfumo wa maisha unavyoweza klusaidia kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa