Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Mohammed Mchengerwa amewataka wasimaizi wa miradi katika Mkoa wa Dar es Salaam kusimamia kwa weledi Miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.
Mhe. Mchengerwa ametoa agizo hilo katika hafla ya utiaji saini Mikataba ya Ujenzi wa Barabara katika Halmashauri Tano za Mkoa wa Dar es Salaam kupitia Mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) iliyofanyika leo Oktoba 24, 2024 katika uwanja vya Mwembe yanga, Manispaa ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam.
“Nawaasa wasimamizi wote, miradi izingatie uhitaji wa eneo husika, washirikisheni wananchi ili wawe na uelewa juu ya miradi hii ili itakapokamilika waweze kushiriki kikamilifu.” amesema Mhe. Mchengerwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake yenye kulenga kuwakomboa Watanzania kiuchumi.
Mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) unatarajiwa kutekelezwa kwa miezi 15 kuanzia Disemba 2024, huku Manispaa ya Kigamboni ikinufaika na ujenzi wa Barabara kwa kiwangocha lami Kilometa 17.78 itakayogharimu zaidi ya Tsh Bil 50
.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa