Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Suleiman Jaffo leo amefanya ziara katika Manispaa ya Kigamboni kukagua ujenzi wa Hopitali ya Wilaya, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na ujenzi wa ofisi ya Halmashauri.
Mhe.Jaffo amepongeza hatua iliyofikiwa na kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kigamboni kwa usimamizi wa karibu na hivyo kumtaka mkandarasi (TBA) kukamilisha ujenzi wa ofisi za Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kabla ya mwezi wa sita mwaka huu 2019.
Aidha Mhe.Jaffo pia ametumia ziara hiyo kuzitaka Halmashauri zote zilizopokea hela za ujenzi wa ofisi, hospitali ya wilaya pamoja na vituo vya Afya kukamilisha ujenzi kwa wakati na kwamba watakaoshindwa watachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na fedha za ujenzi kurudishwa kwa Halmashauri zile ambazo mpaka sasa ujenzi haujaanza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kigamboni Arch.Ng'wilabuzu Ludigija amemhakikishia waziri Jaffo kuwa atahakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuhamia katika Jengo la Halmashauri ifikapo tarehe 25 Juni mwaka huu.
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo pamoja na viongozi wengine wakipata maelezo kutoka kwa mwakilishi wa TBA
Katibu Tawala Wilaya ya Kigamboni Bi. Rahel Mhando akielezea maendeleo ya ujenzi wa ofisi za Mkuu wa Wilaya
msafara wa ziara ukiwa umewasili kwenye eneo la ujenzi wa ofisiza Mkuu wa Wilaya.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa