Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo amewataka wakala wa ujenzi nchini ( TBA) kuongeza kasi ya ujenzi wa jengo la utawala la Manispaa ya Kigamboni kwani muda wa awali waliokubaliana katika mkataba unakaribia kwisha huku wakiwa bado wako katika kiwango cha chini ya asilimia hamsini.
Agizo hilo amelitoa alipotembelea ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigambano linalojengwa na wakala wa Majengo nchini (TBA) katika eneo la Geza ulole kata ya Somangila, ambapo Mhe.Jaffo amemwagiza mkurugenzi kuhakikisha anahamia katika ofisi hiyo ifikapo Januari 2019.
Wakati huohuo Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo amepongeza upanuzi wa kituo cha Afya cha Kimbiji kinachojengwa kutokana na fedha zilizotolewa na ofisi yake katika mpango wa uboreshaji wa huduma za afya nchini.
Mhe. Jaffo amepongeza hatua iliyofikiwa huku akisisitiza ujenzi huo kukamilika ili wananchi waweze kupata huduma iliyotarajiwa na kusema kuwa kwa sasa ofisi yake ipo katika hatua ya kusambaza vifaa katika vituo hivyo ambapo kwa Kimbiji baadhi ya vifaa vimeshapokelewa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda amempongeza Mh. Jaffo kwa jitihada zinazofanywa na ofisi yake katika kuboresha sekta ya Afya nchini kwani katika mkoa wa Dar es Salaam zaidi ya vituo kumi vipo katika mpango huo katika awamu ya kwanza na ya pili.
''Mhe.Waziri, kazi inayofanywa na ofisi yako ni kubwa sana na baada ya muda mfupi wananchi wangu wataanza kunufaika na maboresho haya na kuona matunda ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe.Dr.John Pombe Magufuli" alisema Mhe. amakonda.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ndg Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija amesema ofisi yake itaendelea kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri ikiwa ni pamoja na kuanza upanuzi wa kituo cha Afya cha Kigamboni ambacho mpaka sasa ofisi yake imeshapokea shilingi milioni mia nne kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI.
Katika kituo cha Afya Kimbiji upanuzi umefanyika katika ujenzi wa chumba cha upasuaji, wodi ya akina mama , maabara pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti ambavyo vyote kwa pamoja vitagarimu jumla ya shilingi milioni
Wazir wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Jaffo amefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya Kimbiji na ujenzi wa jengo la utawala akiwa ameambatana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda na uongozi wa Kigamboni kuanzia ngazi ya Wilaya.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Suleiman Jaffo akizungumza na uongozi wa manispaa ya Kigamboni
Viongozi wakitembelea jengo la utawala
Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Sulleiman Jaffo kushoto na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda wakikagua jengo la utawala linalojengwa na TBA
Waziri Jaffo na viongozi wengine wakisikiliza maelekezo ya msisamizi wa ujenzi wa jengo la utawala kutoka TBA(aliyeshika kofia)
Viongozi wakitembelea kuangalia ujenzi wa kituo cha afya Kimbiji
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Suleiman Jaffo akipongeza uongozi kwa ujenzi wa kituo hicho.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa