WAZEE 3518 KIGAMBONI WANUFAIKA NA VITAMBULISHO VYA MSAMAHA WA MALIPO YA MATIBABU,WATAKIWA KUYATUMIA VIZURI MABARAZA
Hayo yamebainika leo katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wazee duniani ambapo Manispaa ya Kigamboni leo 5/10/2022 imeadhimisha katika viwanja vya Mjimwema .
Akiongea Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Fatma Almas Nyangasa ambae pia alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amewapongeza kwa jinsi wanavyotoa ushirikiano kwa uongozi Wilaya kwa kujitokeza pale wanapoitwa na amesisitizabkuwa serikali inawatambua na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu anawathamini na anatambua mchango wao katika taifa hili na inathamini pia amewataka kuyatumia vizuri mabaraza ya wazee kwa kushirikiana na watendaji katika Kata zao.
Akiongelea kuhusu maombi mbalimbali yaliyoainishwa katika risala yao DC Nyangasa amesema kuwa ameyachukua kwa ajili ya kuyafanyia kazi.Aidha amemshukuru Mkurugenzi ndg.Kiwale kwa utekelezaji wa maagizo mbalimbali ambayo amekuwa akimpa kuhusiana na maswala yao wazee.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni ndg.Erasto Kiwale ameeleza kwa jinsi Manispaa inavyotekeleza maagizo ya Serikali kuhusiana na maswali ya wazee likiwepo suala la kutoa vitambulisho vya msamaha wa malipo ya matibabu kwa wazee ambapo wazee 3518 wamepatiwa vitambulisho hivyo.
Aidha amesema Manispaa imekuwa ikitoa elimu ya Chanjo ya COVID -19 kwa wazee ambapo wazee 2228 wamepata elimu hiyo,pamoja na hilo Manispaa imesimamia uundaji wa mabaraza 77 kwa wazee kuanzia ngazi ya Wilaya, Kata na mtaa,aidha Manispaa imeendelea kutoa elimu ya saikolojia kwa wazee na kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ilifanikiwa kutumia mil.7.4 kuwakatia bima wazee kwa ajili ya unafuu wa matibabu.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini KGMC
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa