Katika sherehe hizo, jamii ya Kigamboni ilijitokeza kufanya usafi na kupanda miti katika soko la Kibada, ikiwa ni sehemu ya kuchangia maendeleo endelevu. Aidha, mashindano ya kitaaluma na michezo yalifanyika, ikiwemo uandishi wa insha kwa wanafunzi wakijikita kwenye kauli mbiu, "Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo".
Mashindano ya soka yalihusisha timu za Vijibweni FC na Kigamboni Soccer Academy, huku mchezaji wa soka la wanawake, Rahma Ramadhani wa Tungi, akiahidiwa kufadhiliwa vifaa vya michezo na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni. Sherehe hizi zilitumika kuhamasisha uzalendo, bidii kazini, na mshikamano wa kijamii
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa