Ni kauli ya makamu wa Rais Mhe. Samia Hassan Suluhu alipokuwa akizungumza na wananchi leo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa tanki la maji linalojengwa Kisarawe II Wilayani Kigamboni linalohusisha visima 12 na uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 15 linalojengwa kwa kutumia fedha za ndani za DAWASA kiasi cha Bilioni 23.
Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali imejitoa kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji kwa kutumia gharama kubwa kujenga miundombinu ya maji ili kustawisha afya na maendeleo ya wananchi, Hivyo wananchi wa Kigamboni wanapaswa kuilinda miundombinu hiyo wakati wa utekelezaji wa mradi na hata baada ya kukamilika ili lengo lililokusudiwa liweze kukamilika.
“ Wapo wananchi ambao walichimba visima vya maji na kusambaza kwa wananchi wengine kwa lengo la kuuza , Serikali inapoleta maji ya gharama nafuu wauza maji hao wanabeza ,hii haipendezi naomba wauza maji msituharibie Siasa nguvu iliyoweka Serikali kutatua changamoto ya maji ni kubwa”
Ameongeza kwa kuwataka Watendaji wa Mitaa kuunda kamati za maji zitakazokuwa na jukumu la kulinda miundombinu ya maji iliyopo katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kusimamia changamoto ya kubambikiwa kwa gharama za bili ya maji wanazopata wananchi kutoka DAWASA.
Mhe. Samia amesema kuwa anaimani hadi kufikia Desemba tatizo la maji Dar es Salaam litakuwa limekwisha nakuwataka Wizara ya Maji kumaliza tatizo la maji kwa kukamilisha miradi inayojengwa nchi nzima isiwe kwa Dar es Salaam pekee ili lengo la Serikali la hadi kufikia 2025 utatuzi wa changamoto ya upatikanaji wa maji nchini liwe limekamilika.
Aidha Mhe. Samia ameitaka kampuni inayotekeleza ujenzi wa mradi wa maji Kisarawe II Advent Construction Limited kukamilisha mradi kwa wakati na kwa viwango vinavyoptakiwa ili wananchi waweze kunufaika na mradi huo .
Mradi wa ujenzi wa Tanki la maji linalojengwa kisarawe II unatarajiwa kumalizika November na unahusisha visima 12 ambapo hadi sasa visima 7 tayari vinafanya kazi
Ujenzi wa tanki la maji ukiwa katika hatua za awali
Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Cpriyan Luhimija akielezea namna mradi huo utakavyonufaisha wakakzi wa kigamboni na maeneo ya Jirani kama Kongoe na Mbagala kwa Makamu wa Rais.
Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Cpriyan Luhimija akitolea ufafanuzi hatua ya ujenzi wa tanki hilo na namna walivyojipanga kulikamilisha kwa wakati.
Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu akiwa anazungumza na Waizri wa Maji Juma Aweso mara baada ya kukagua mradi
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Sara Msafiri akizungumzia kwa uchache namna Wilaya ilivyo na matarajio na mradi huo na utakavyonufaisha wakazi wa Kigamboni.
Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Cpriyan Luhimija akitolea ufafanuzi jinsi DAWASA ilivyojipanga kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji Kigamboni na Dar es Salaam kwa ujumla.
Makamu wa Rais na Viongozi wengine wakiendelea kupokea ufafanuzi jinsi DAWASA ilivyojipanga kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji Dar es Salaam.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa