Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndugu Erasto Kiwale amewataka wataalamu wa Idara ya Ardhi Manispaa ya Kigamboni kuepuka kutoa majibu mepesi wakati wa kutatua kero za Wananchi haswa zinazohusu migogoro ya Ardhi.
Ndugu, Kiwale ametoa wito huo asubuhi ya leo tarehe 12/02/2022 wakati akifungua zoezi la kusikiliza na kutatua kero zinazohusu urasmishaji lililofanyika Ofisi ya Kata ya Mjimwema ambapo Wananchi wa mtaa wa Mjimwema, Magogoni, Ungindoni pamoja na Maweni walipata fursa ya kuwasilisha kero zao.
Aidha akitilia msisitizo amezitaka Kampuni binafsi zinazofanya urasimishaji kuweka wazi mikataba yao kwa Wananchi pamoja na kuepuka chelewesha mchakato mzima wa urasimishaji ili kupunguza malalamiko.
Sambamba na hilo Mratibu wa Urasimishaji Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Laulent Luswani ameeleza kuwa wameandaa utaratibu wa kuzunguka kila Wilaya kwa lengo la kutatua Kero zinazohusu urasmishaji kwa Mkoa wa Dar es Salaam
Akifunga zoezi la kusikiliza kero Kamishna Msaidizi wa Ardhi kanda ya Dar es Salaam Ndugu Idrisa Kayela pia amezitaka Kampuni zinazofanya urasimishaji kutoa elimu ya Upimaji kwa Wananchi ili kuepuka malalamiko yasiyo ya lazima kwa Wananchi.
Aidha amewapongeza Watumishi wa Idara ya Ardhi kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato kwani mwamko wa ulipaji wa kodi ya Ardhi umekuwa mkubwa kwa Manispaa ya Kigamboni.
Zoezi la kusikiliza kero zinazohusu urasmishaji limeenda Sambamba na utoaji wa Hati Miliki ambapo jumla ya Hati 170 zilitolewa kwa Wananchi
Kamishna Msaidizi wa Ardhi kanda ya Dar es Salaam akigawa Hati Miliki kwa Wananchi
Mwananchi akiwasilisha kero zinazohusu urasmishaji katika Mtaa wa Mjimwema, Magogoni, Ungindoni, na Maweni.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa