WATUMISHI MANISPAA YA KIGAMBONI WATAKIWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEJELEZAJI WA MAJUKUMU YAO
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg.Erasto Kiwale amewataka watumishi wa Manispaa hiyo kufuata Sheria na Kanuni katika kutekeleza wajibu wao.Akiongea katika Mkutano uliofanyika Leo wa uongozi wa Manispaa hiyo na watumishi wote uliokuwa na lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali za watumishi ili ziweze kutatuliwa.
Ndg.Kiwale amesema kuna kanuni na Sheria ambazo kwa vyovyote vile mtumishi anatakiwa na anawajibika kuzifuata kwani ndio muongozo wa utekelezaji wa majukumu katika eneo la kazi akitolea mfano kanuni ya Kuwahi kufika kazini kwa wakati ni kanuni ambayo kila mtumishi anatakiwa atekeleze na kufika kufanya majukumu yake ili kuepuka kuvunja kanuni hiyo.Akiongelea suala la kufika kazini kwa wakati amesema kila mtumishi ana wajibu wa Kuwahi kufika kazini kwa wakati ,muda wa kufika kazini umeweka kisheria,hivyo mtumishi hatakiwi kufika muda anaoutaka yeye.
Pia amesisitiza mfumo rafiki kati ya wakuu wa idara wakati ambapo mtumishi anaomba ufafanuzi kuhusu Jambo au anapompelekea shida inayohitaji utatuzi ili kufanya eneo la kazi kuwa sehemu salama na penye Amani, pia amesisitiza suala la watumishi kuwahudumia wananchi wanaokuja kufata huduma kwa weledi bila kuwanyanyasa au kutumia lugha mbaya.
"Katika utekelezaji wa majukumu yenu kuna kanuni zinazowaongoza ambazo mnawajibika kuzifuata na si kuzikwepa ili kuwe na ufanisi,usalama na Amani katika eneo la kazi hivyo hamna budi kuzifuata."alisema ndg.Erasto Kiwale.
Nae Afisa Utumishi Mkuu Bi.Florah Malima akiongelea suala la kufata utaratibu na kanuni katika utekelezaji wa majukumu katika mengi aliyoongelea amegusia pia suala la utaratibu wa kuombabkibali cha malipo ya masaa ya ziada ambapo amesema Mkuu wa Idara ana wajibu wa kuomba kibali pale ambapo anajua kutakuwa na kazi itakayowataka watumishi katika idara yake kufanya kazi katika muda wa ziada ili kuweza kufuata utaratibu wa kuwaimbea stahiki zao wale watakaofanya kazi hizo nje ya muda wa kazi na si kuamua tu bila kufuata utaratibu ulioelekezwa.
Akiongea Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa Bi.Shamila Hassan wa TALGU ambao walialikwa kwenye Mkutano huo wamempongeza Mkurugenzi kwa utaratibu huu aliojiwekea wa kukutana na watumishi wa Manispaa yake kwa ajili ya kusikiliza changamoto walizo nazo ili kuzitaftia ufumbuzi .
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni ameweka utaratibu wa kukutana na Watumishi wake mara moja katika kila robo ya mwaka ili kusikiliza changamoto walizo nazo ili zifanyiwe kazi na pia kutoa msisitizo katika suala la kuwajibika bila shuruti.
IMETILEWA NA KITENGI CHA HABARI NA MAWASILIANO MANISPAA YA KIGAMBONI
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa