Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Arch.Ngwilabuzu Ludigija leo tarehe 23 amewatoa wasiwasi waheshimiwa Madiwani wakati wa kuhitimisha kikao cha baraza kuhusiana na sula la kuhamia kwenye ofisi mpya zinazojengwa Gezaulole Kata ya Somangila na mikakati ya kuhakikisha idadi ya shule za kidato kidato cha tano zinaongezwa.
Akijibu hoja ya Diwani wa Vijibweni kuhusiana na ni lini watumishi watahamia kwenye jengo jipya la utawala Mkurugenzi Ludigija amesema kuwa tarehe 30 mwezi huu ndio tarehe rasmi ya kuhamia lakini zipo baadhi ya Idara ambazo hazina vikwazo vya kuhamia mapema kwenye jengo hilo hivyo kuanzia jumatatu ya tarehe 26 wiki ijayo watakuwa wanahamia huku Idara nyingine zikisubiri ukamilikaji wa miundombinu itakayowawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Aidha kuhusiana na suala la kuongeza shule za levo ya juu yaani kidato cha tano na sita Mkurugenzi amesema kuwa Manispaa inampango wa kuipandisha hadhi shule ya Kisarawe II Sekondari, Kigamboni pia inatazamiwa kuona ni namna gani inaweza kupata shule ya kidato cha tano na mikakati mingine ya kupandisha hadhi na kujenga baadhi ya shule ili kuondoa upungufu wa kuwa na kidato cha tano kwenye Shule ya Nguva pekee.
Baraza la Madiwani limehitimishwa leo ambapo waheshimiwa Madiwani wameliridhishwa na majibu ya Mkurugenzi yaliyotokana na maswali ya papo kwa papo.
Mkurugenzi Arch.Ng'wilabuzu Ludigija akijibu hoja za madiwani kuhusu shule na kuhamia ofisi mpya za Manispaa
Diwani wa Kata ya Vijibweni Mhe. Isaya Mwita akiuliza swali la mikakati ya kuongeza shule za kidato cha tano na sita
Viongozi na wageni waalikwa wakifatilia mkutano wa baraza kwa makini
Diwani wa Viti Maalum Mhe. Amina Yakoub akiuliza swali la lini watumishi watahamia kwenye ofisi mpya za Manispaa.
muonekano wa Jengo la utawala kwa nje likiwa kwenye hatua za umalizizaji.
Muonekano wa ofisi kwa ndani zikiwa kwenye hatua za umaliziaji
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa