Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Almasi Nyangassa ameashukuru wanawake kutoka Mamlaka ya Bandari Dar es Salaama kwa msaada wa bima za afya 100 za NHIF zilizotolewa kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa lengo la kuwasaidia kimatibabu.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano leo kwenye ukumbi wa Ofisi za Mkuuu wa Wilaya, Mhe Fatma amesema kuwa Serikali ikipata sapoti za wadau inarahisisha kutatua changamoto haraka zaidi kama bima walizozitoa kwani zitawasaidia watoto kupata huduma za msingi za kiafya na kwa urahisi zaidi.
Ameongeza kwa kusema kuwa kitendo walichofanya wanawake wa mamlaka ya bandari ni ishara ya kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhakikisha kila mwananchi anakua na Bima ya afya kama ambavyo siku za usoni serikali ilivyodhamiria kuhakikisha wananchi wote wanakua na Bima za afya.
“Nawashukuru sana wanawake wa TPA kwetu hili ni jambo kubwa sana, Kigamboni tunakundi kubwa la watu wanaohitaji msaada wa namna hii kwani mmetusaidia kwanza, kwa kuunga mkonojitihada za Serikali lakini pia hii imedhihirish upendo alionao mama kwa mototo kwani mngeweza kufanya jambo lingine lolote na mahali kwingine lakini mkaona vyema kuwafikia watoto wa Kigamboni “Alisema Mkuu wa Wilaya
Akizungumza wakati wa makabidhiano kaimu meneja Rasilimali watu Mwajuma Mkonga kutoka Mamlakaya Bandari amesema kuwa , katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani wameamua kuangaza tabasamu kwa watoto wanaoishi mazigira magumu na walezi wao kwa kuwalipia Bima za NHIF zitakazowasaidia kupata matibabu kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Ameongeza kwa kusema kuwa walikusanya fedha kutoka kwa watumishi na wadau mbalimbali ambazo zimesaidia kununua bima 400 kwa lengo la kukabidhi kwa wilaya 3 za Dar es Salaam na fedha nyingine zimetumika kutoa msaada kwa Hospitali za Temeke na MMuhimbili
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyangassa akizungumza Mara baada ya makabidhiano ya Bima za Afya Kushoto ni Kaimu Rasilimali watu kutoka Mamlaka ya Bandari Bi. Mwajuma Mkonga
Mkuu wa Wilaya Mhe.Fatma Nyangassa akiwashukuru wanawake kutoka mamlaka ya bandari, pembeni ni Kaimu Meneja rasilimali watu Mwajuma Mkonga.
Baadhi ya wanawake wa mamlaka ya Bandari waliofika kukabidhi Bima za Afya kwa watoto.
Mkuu wa Wilaya Mhe.Fatma Nyangassa akipokea zawadi kutoka kwa kaimu meneja rasilimali watu kutoka mamlaka ya bandari Bi.Mwajuma Mkonga.
Baadhi ya watoto waliowawakilisha watoto wenzao wakati wa makabidhiano ya Bima za Afya.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Wilaya Mhe.Fatma Nyangassa na wanawake kutoka mamlaka ya bandari Mara baada ya makabidhiano.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa