Watoa huduma wa Afya ngazi ya jamii 67 wajengewa uwezo wa mafunzo ya ulishaji wa watoto wadogo kuanzia mama anapokuwa mjamzito ,mtoto anapofikisha umri wa miezi 6 -24 ili kuwasaidia kutoa elimu inayohitajika kwa jamii kwa lengo la kupunguza hali ya utapiamlo.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo kwenye ukumbi wa Manispaa Afisa lishe wa Wilaya Bi.Henerietha Henry amesema kua, lishe bora inaanzia kipindi mama anapokua mjamzito kwasababu mtoto anaanza kupata chakula kupitia milo anayokula mama yake hivyo ni vyema kuzingata ulaji sahihi ili kumjenga mtoto tangu akiwa tumboni.
Akiongelea kuhusu elimu ya lishe na upungufu wa damu kwa waamama wajawazito Afisa lishe amesema kuwa vyakula vyenye asili ya mimea na wanyama ni muhimu kuvizingatia ikiwemo na matumizi sahihi ya dawa za kuongeza damu wanazopewa kliniki ili kumuwezesha kujifungua mtoto mwenye afya bora.
Akizungumzia suala la unyonyeshaji wa watoto mara baada ya mama kujifungua kwa kipindi cha miezi sita afisa lishe amewasisitiza watoa huduma za afya kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa maziwa ya mama pekee kwa kipindi hicho kwani yanajitosheleza na yanavirutubisho vyote anavyopaswa kuvipata mtoto.
Aidha amewaeleza watoa huduma kuelimisha jamii kuwa maziwa ya mama asilimia70 ni majimaji hivyo ile dhana ya maziwa mepesi na kuona watoto hawashibi waiondoe kwani kumuanzishia chakula mbadala katika kipindi cha miezi 6 kunaathari kubwa.
Akizungumzia faida ya kumnyonyesha mtoto miezi 6 bila kumpatia chakula mbadala Afisa lishe amesema kuwa, maziwa ya mama ni Kinga tiba, sio gharama na yanajitosheleza . chakula mbadala kwa mtoto chini ya miezi 6 kunaweza kupelekea kupata magonjwa sugu kama kisukari na presha , uwezekano wa kupata aleji, athari katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula sababu haujakomaa na maradhi mengineo.
Kwa upande wa elimu ya ulishaji wa watoto kuanzia umri wa miezi sita hadi miezi ishirini na nne Afisa Lishe Fauzia Msuya amesema kuwa ni muhimu kwa wazazi au walezi kuzingitia kumpatia mtoto nishati inayohitajika kulingana na umri wake kwa kuzingatia makundi maalumu yoe ya chakula.
Mafunzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa na kuhudhuriwa na watoa huduma wote kutoka mitaa 67 ya Manispaa ya Kigamboni.
Afisa lishe wa Wilaya Bi.Henerietha Henry akitoa mafunzo ya ulishaji kwa watoto kuanzia wakiwa tumboni mwa mama zao kwa watoa huduma ngazi ya jamii kwenye ukumbi wa manispaa
watoa huduma ngazi ya jamii wakisikiliza kwa umakini mafunzo yanayotolewa na Afisa lishe.
Mmoja wa watoa huduma ya Afya ngazi ya Jamii akichangia mada ya athari za kumuanzishia mtoto chakula mbadala kwa kipinddi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa.
Watoa huduma ya afya ngazi ya jamii wakifuatilia mafunzi ya lishe bora kwa mama mjamzito ili kuimarisha ulishaji wa mtoto akiwa tumboni.
Watoa huduma ya Afya ngazi ya jamii wakifuatilia kwa umakini mafunzo ya ulishaji kwa watoto.
Mmoja wa watoa huduma ya Afya ngazi yajamii akichangia faida za unyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa watoto kipindi cha miezi 6.
Watoa huduma ya Afya ngazi ya jamii wakifuatilia mafunzo.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa