Serikali wilayani Kigamboni imewaagiza watendaji kusimamia kwa weledi uzoaji wa taka ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kutokana na taka hizo.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Halima Bulembo leo Septemba 26, 2023 alipozungumza na mama na baba lishe katika mtaa wa Mwasonga na kupokea hoja kutoka kwa mmoja wa mama lishe anayetambulika kwa jina la Asha Mfaume anaefanya shughuli zake katika eneo la mwasonga "center" ya kutokuwepo kwa kizimba cha kukusanyia taka.
Kutokana na hali hiyo, DC Bulembo akawaagiza Watendaji wa Kata na Mitaa iliyopo Kisarawe II kuzingatia usafi wa mazingira sambamba na kutenga eneo maalum la kukusanyia taka.
Sambamba na hilo Mhe. Bulembo amewaonya wanawake kutojihusisha na mikopo ijulikanayo kama kausha damu na kwamba haina tija na zaidi inawaongezea gharama za maisha tofauti na matarajio yao ya kujiinua kiuchumi.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa