Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Halima Bulembo amewataka watendaji wa Kata, watendaji wa Mitaa pamoja na Wenyeviti wa Serikalini za Mitaa 67 ya Manispaa ya Kigamboni kusikiliza na kutatua kero za Wananchi katika maeneo yao.
Mheshimiwa Bulembo ametoa agizo hilo leo Agosti 20. 2024 katika kikao chake na watendaji hao pamoja na wenyeviti kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kigamboni kwa lengo la kutoa maelekezo juu maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.
Aidha katika kikao hicho DC. Bulembo amesema tarehe 09/09/2024 anatarajia kufanya ziara ya Mtaa kwa Mtaa kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za Wananchi katika kata zote za Manispaa ya Kigamboni
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa