Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni na Mkuu wa Idara ya kilimo mifugo na uvuvi Bi. Priscila Muhina amewataka watendaji wa Kata na Mitaa pamoja na Maafisa ugani kutoa elimu kwa Wananchi juu ya ufugaji wa mjini huku wakiwaasa kuacha tabia ya kuachia mifugo yao kuzurura hovyo.
Bi. Priscila Muhina ametoa agizo hilo asubuhi ya leo Februari 14. 2024 alipomuwakilisha Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni Ndugu Erasto Kiwale katika kikao cha kamati ya lishe cha robo ya mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi mkubwa wa Manispaa ya Kigamboni kwa lengo la kujadili na kupitia shughuli mbalimbali za lishe katika kipindi cha robo ya pili
Katika kikao hicho Bi. Priscila amewataka watendaji na maafisa ugani kusimamia sheria kanuni na taratibu za ufuagaji wa mjini ili kuepuka migogoro inayoweza kutokea kutokana na tabia ya baadhi ya wafugaji kuachia mifugo yao kuzurura hovyo.
Kwa upande mwingine kamati ya lishe ya Manispaa imemuagiza Afisa Lishe wa Manispaa ya Kigamboni Bi. Anna Byashara kuendelea kufanya utambuzi na kutoa elimu kwa wamiliki wa Mashine za kusaga nafaka kuweka virutubishi kwenye bidhaa wanazozalisha.
Aidha imewataka Maafisa elimu Msingi na Sekondari wa Manispaa kuwaagiza walimu wakuu wa shule wanazozisimamia kuanzisha klabu za lishe kwa lengo la kutoa elimu kwa kamati za shule na wanafunzi wa shule hizo.
Sambamba na hilo kimewataka watendaji wa Kata kuweka agenda ya lishe katika vikao vya maendeleo ya Kata (WDC) ili kuongeza wigo wa utoaji wa elimu kwa Wananchi
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa