Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Halima Bulembo amewataka watendaji wa Kata, Mitaa pamoja na Maafisa Afya ngazi ya Kata kusimamia usafi katika maeneo yao ili kuepuka magonjwa ya Mlipuko yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
DC Bulembo ametoa agizo hilo leo Aprili 17. 2024 katika kikao kazi kilichohusisha watendaji wa kata na Mitaa, Maafisa Afya, Maafisa Masoko pamoja na Maafisa mazingira ngazi ya kata na Wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi yake kwa lengo la kupokea tathmini ya athari za Mvua pamoja na tahadhari ya magonjwa ya Mlipuko Wilayani humo.
Katika kikao hicho DC Bulembo amewataka watendaji hao kusimamia sheria za usafi na kuhakikisha wanashikiana na Wananchi ili kufanya usafi katika maeneo ya makazi na ya umma pia aliwataka wataalamu wa Idara ya Afya kupulizia dawa katika maeneo hatarishi ili kuuwa vimelea vinavyoweza kuleta magonjwa ya Mlipuko.
Hata hivyo baada ya kikao hicho Mkuu huyo wa Wilaya alifanya ziara katika eneo la Minazi Mikinda ambapo alizungumza na Wananchi wa eneo hilo na kuwataka kuzingatia usafi katika shughuli zao za kila siku ikiwa ni hatua muhimu ya kuchukua ili kujikinga na magonjwa ya Mlipuko
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa