Kaimu wa Divisheni ya utawala na usimamizi wa rasilimali watu Manispaa ya Kigamboni Ndugu Goodluck Kavishe amewataka watendaji wa Mitaa 67, waratibu elimu kata, watoa huduma ya Afya ya mama na Mtoto pamoja na Walimu wanaoshughulikia taarifa za TASAF kwa shule za Msingi na Sekondari kusimamia kwa weledi zoezi la uingizaji wa taarifa za wanufaika wa mradi wa kunusuru kaya maskini (TASAF) ili kuepuka malalamiko yasiyo ya lazima.
Ndugu Goodluck Kavishe ametoa wito huo leo Julai 18. 2024 katika kikao kazi cha watendaji hao kilichoandaliwa na kitengo cha TASAF kwa lengo la kuwajengea uelewa na uwezo juu ya mradi huo ambapo alimuwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndugu Erasto Kiwale.
" lengo la mafunzo haya ni kujenga na sio kubomoa au kuzalisha malalamiko." Alisema Kaimu huyo.
Aidha alitumia nafasi hiyo kuwataka watendaji na wataalamu hao kufanya kazi kwa ushirikiano ili zoezi hilo liweze kukamilika kwa wakati.
Kwa upande mwingine mshauri wa mradi wa kunusuru kaya maskini (TASAF) Manispaa ya Kigamboni Bi Sekela Komba amewataka watendaji hao kufuata sheria kanuni na taratibu zote za ulipaji wa walengwa ili kuepuka hoja zisizo za lazima.
Aidha aliwataka kutenda haki huku akiwaasa kusimamia vizuri zoezi hilo na kutoa malipo kwa walengwa kulingana na Mitaa yao.
@halima_bulembo @erastokiwale2011 @ernestmafimbo @ikulu_mawasiliano @samia_suluhu_hassan @ortamisemi @tasaf.tanzania @daressalaam_rs_digital @ccmtanzania @ccm_kigamboni
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa