Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Kigamboni Ndg.Charles Lawisso Leo amefungua mafunzo ya Mfumo wa NAPA awamu ya pili kwaajili ya kuwajengea uwezo Watendaji wa Kata,Mitaa na Wakusanya data kuweza kutekeleza vyema Uhakiki wa Anwani za Makazi.
Akifungua mafunzo hayo leo kwenye ukumbi wa Manispaa amewasisitiza washiriki hao kuwa makini ili zoezi la Uhakiki wa Anwani liweze kutekelezeka kwa ufanisi.
Aidha ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi wa Kigamboni kufika kwenye ofisi za za Mitaa ili kuweza kuhakiki taarifa zao na kufanya marekebisho ikiwa yatakuwepo.
Ameendelea kwa kusema kuwa Anwani za makazi ni zoezi linaloendelea likilenga kurahisisha zoezi la Sensa ya watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika August 23 , pia Anwani hizi zitarahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mafunzo hayo yamewezeshwa na Maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wizara ya Habari na mawasiliano.
TAARIFA ZA ANWANI ZIMEBANDIKWA KWENYE OFISI ZA MITAA YOTE 67 ,MWANANCHI SHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE UHAKIKI WA ANWANI ZA MAKAZI.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg.Charles Lawisso akisisitiza washiriki kuwa makini na mafunzo.
Washiriki wa mafunzo ya Mfumo wa NaPA awamu ya Pili.
Mratibu wa Anwani za Makazi Wilaya ya Kigamboni Bib.Magdalena Malunda akitoa maelekezo kwa washiriki.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo
Mkufunzi kutoka wizarani akitoa mafunzo ya mfumo we NaPA kwa washiriki.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa