Matukio yaliyojiri katika kikao kazi cha kuutambulisha Mradi wa uboreshaji usalama wa Milki za Ardhi unaodhaminiwa na Benki ya Dunia kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Kigamboni leo Septemba 19. 2023.
Katika kikao hicho Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mheshimiwa Ernest Mafimbo amewataka wataalamu wa Idara ya Ardhi kuchukua hatua za haraka katika kuutekeleza mradi huo ili Wananchi waweze kuona matunda.
"Sisi kama Madiwani tupo tayari kuhamasisha Wananchi kupitia vikao vya Kata pamoja na Mikutano ya hadhara kwani nia yetu ni kutaka Mkoa wa Dar es Salaam upangike" Alisema Mheshimiwa Mafimbo
Pia aliwataka kuufanya mchakato wote wa utekelazi kwa vitendo kwa lengo la kuhakikisha Mradi unaanza mapema kulingana na muda uliopangwa
Akieleza faida za Mradi huo Kamisha wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu. Shukuran Kyando amesema mradi utasaidia kutatua changamoto za Migogoro ya Ardhi pamoja na kukomesha utapeli unaofanywa na baadhi ya watu ambao sio waaminifu.
Mradi wa uboreshaji usalama wa Milki za Ardhi unatarajia kutekelezwa katika Mkoa wote wa Dar es Salaam ambapo utalenga kurasimisha zaidi ya viwanja 3,354
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa