Msimamizi wa uchaguzi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Ndugu. Erasto Kiwale amewataka watendaji wa Kata na Mitaa ambao ni wasimamizi wasaidizi kuzingatia maadili ya Utumishi wa umma ili kuzuia makosa yasiyo ya lazima katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27. 2024.
Ndugu Kiwale ametoa wito huo leo Septemba 30. 2024 katika mafunzo ya wasimamizi wasaidizi hao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi yake kwa lengo la kupitia kanuni taratibu na muongozo wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
" unapofanya kazi ya uchaguzi jua ni swala la kikatiba lenye miongozo kanuni na taratibu zake hivyo ni muhimu kuzizingatia ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima." Alisema Ndugu Erasto Kiwale.
Aidha alitumia nafasi hiyo kuwataka watendaji hao kuwa wazalendo huku akiwaasa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili uchaguzi uwe huru na wa haki.
Hata hivyo aliendelea kusisitiza kwa kuwataka kuzingatia ratiba ya matukio yote muhimu katika uchaguzi huo na amewasihi kutunza na kuhifadhi vizuri vifaa vyote vitakavyotumika katika zoezi hilo.
Mafunzo hayo yalihusisha watendaji wa Kata 9 Mitaa 67 pamoja na waratibu 10 wa uchaguzi ambapo maada mbalimbali ziliwasilishwa na kujadiliwa.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa