Mratibu wa Maafa Wilaya Bi. Suzan Swai amewakumbusha wajumbe wa kamati za maafa wanaowakilisha Kata za Kigamboni kufanya kazi kwa kuzingatia majukumu yao na kuwa mabalozi kwa jamii zinazowazunguka pindi majanga ya moto na mengineyo yanapotokea.
Mratibu wa Maafa ameyasema hayo leo alipokuwa akizindua kamati za maafa zilizoambatana na mafunzo ya kinga na tahadhari ya moto yaliyoendeshwa na Afisa Zimamoto Wilaya kutoka Jeshi la Zimamoto na uokoaji Inspekta Castory Willa kwenye ukumbi wa Manispaa.
Aidha Afisa Zimamoto amesisitiza umuhimu wa kila mwananchi kuwa na namba za zimamoto za dhalura yaani 114 , wananchi kuwa na Bima za majanga ili lengo la kuokoa mali na Maisha pindi majanga yanapotokea liweze kutimia , pia jeshi la zimamoto linatoa ushauri wa namna bora ya kujenga ili kukabiliana na majanga hususani ya moto.
Jeshi la zimamoto pia limekabidhi vifaa vya awali vya kuzima moto kwa kata tatu za Kisarwe II, Kimbiji na Pembamnazi.
Wakufunzi wa mafunzo ya zimamoto na wajumbe wa kamati za maafa Kata wakiwa tayari kufanya majaribio ya kuzima moto kwa ktumia njia tatu.
Mratibu wa Maafa Wilaya Bi Susan Swai akimkabidhi kifaa cha kuzimia moto cha awali mratibu wa Maafa ngazi ya Kata , Kata ya Pembamnazi
Zoezi la kuzima moto kwa kutumia mtungi wa gesi likifanyika
Mkufunzi wa mafunzo ya kinga na uzimaji moto kutoka kikosi cha zimamoto Insp. Castory Willa akionesha namna ya kutumia mtungi wa foam kuzima
Wawakilishi wa waratibu wa Maafa na wakufunzi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Mafunzo.
Mwakilishi wa waratibu wa Maafa akizima moto.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa