Katika kutekeleza wa maagizo ya Serikali Manispaa ya Kigamboni leo imefungua jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi ambalo lilianzishwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu ambapo mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bi.Rahel Muhando alishiriki kuzindua jukwaa hilo Ngazi ya Kata na kuwasisitiza wanawake kujiunga kwenye vikundi ili waweze kunufaika na mikopo inayotolea na Manispaa.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa jukwaa Kata ya Kibada Bi. Rahel Mhando (Katibu Tawala Wilaya) alisema kuwa huo ni mwendelezo na ni utekelezaji wa agizo la Serikali kwamba ngazi ya Wilaya, Kata na Mitaa kote kuwe na majukwaa ya uwezeshaji wanawake ambapo lengo kuu likiwa ni kuwawezesha Wanawake kujikwamua kiuchumi, kupitia asilimia 10 za mapato ya ndani zinazotolewa na Manispaa inayohusisha pia Vijana na walemavu katika kuwawezesha kujikwamua na umasikini.
Aliongeza kuwa katika ziara aliyoifanya takribani maeneo yote ya Kigamboni amegundua kuwa wakinamama wengi wameitikia wito wa kujiunga katika vikundi ambapo sasa ni jukumu la Serikali kuhakikisha fedha zinazotengwa zinawafikia walengwa kwa wakati.
“Nawasisitiza wanawake muendelee kujiunga kwenye vikundi ili muweze kufikiwa kwa urahisi kwenye mikopo hata na tasisi ambazo zimejitoa kusaidia kuwainua kiuchumi, vijana pia mjiunge kwenye vikundi Serikali ipo kuwahudumia na sisi Kigamboni tumejipanga kutekeleza agizo la Serikali” alisema Bi.Rahel
Kwa upande wake mlezi wa jukwaa la wanawake Kata ya Kibada ambaye pia ni Diwani wa Kata hiyo Mhe. Amin Mzuri Sambo alisema kuwa ni jambo la faraja kuona wakinama wanajikwamua kiuchumi na kuwataka kutumia vyema fursa ambayo Serikali imeitoa kwao kwasababu wao kama viongozi wapo kuhakikisha fedha tengwa zinawafikia walengwa wote wakiwemo vijana na walemavu.
Uzinduzi wa jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi Kata ya Kibada lenye kauli mbiu ya “Wanawake tumieni fursa ya jukwaa kushiriki uchumi wa viwanda” ni muendelezo ambapo mpaka sasa Kata 6 kati ya 9 zimekwishazindua majukwaa.
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ilitenga kiasi cha milioni 311 kwaajili ya mikopo ya vijana na wanawake na kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Manispaa imetenga Milioni 537 kwaajili ya mikopo ya wanawake na vijana na milioni 132 kwaajili ya waalemavu.
Katibu Tawala Wilaya Bi.Rahel Mhando akiwa ameambatana na wanawake akikakua bidhaa mbalimbali
Wanawake wajasiliamali wakimshangilia mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala Wilaya.
Mlezi na diwani wa kata ya Kibada Mhe. Mzuri Sambo akizungumza na wanawake kwenye uzinduzi wa jukwaa
Viongozi wakiwa wamesisima kutazama vikundi vyakinamama vikipita kutoka mitaa mbalimbali ya kata ya kibada.
Wanawake wakiwa kwenye shamrashamra
moja ya mtaa wa Kibada ukipita na bango lake mbele ya viongozi ili wapate kusoma ujumbe.
Vijana wa hamasa wakisherehesha
Katibu Tawala Wilaya Bi.Rahel Mhando akikagua bidhaa za batiki kutoka moja ya kikundi cha kinamama
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa