"Niwatie moyo Wanawake wenzangu tuwe na umoja na umoja wetu usiwe wa kutakiana mabaya bali tushirikiane."
Kauli hiyo imetolewa leo na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Bi. Dalmia Mikaya (Katibu Tawala Wilaya ya Kigamboni) alipokuwa akikabidhi msaada wa Mifuko ya sukari, katoni za maji, sabuni za kufulia, sabuni za mche, mchele, unga wa sembe unga wa ngano, maji ya kunywa kalamu, mabegi ya shule pamoja na vifaa vya usafi. Vilivyokabidhiwa kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Hisani kilichopo Kata ya Kibada Manispaa ya Kigamboni.
Aidha katika tukio hilo Bi. Dalmia aliwataka Wanawake wa Kigamboni kujivunia nafasi yao katika jamii hususani katika kuleta maendeleo ya Taifa kwani Mwanamke anamchango mkubwa.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa Bi Happy Luteganya amesema lengo la kutoa msaada huo ni kutambua changamoto ya watoto yatima na njia moja wapo ya kuadhimisha siku ya Mwanamke katika Wilaya ya Kigamboni kwa vitendo.
Siku ya mwanamke duniani husheherekewa tarehe 8 mwezi Machi kila mwaka na mwaka huu imeongozwa na kauli mbiu isemayo Wanawake katika uongozi ni chachu kufikia dunia ya usawa.
Katibu Tawala Wilaya ya Kigamboni akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha Hisani
Baadhi ya watoto ambao ni yatima katika kituo cha Hisani wakipokea msaada.
Mkuu wa Idara ya maendeleo ya jamii akitoa neno kwa niamba ya Mkurugenzi
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa